Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 28 Desemba 2014

Huu ni Mfuniko wa aina yakee..Tizama Tamasha la tuo8january mjini Morogoro!! Ngumu na Laini zote zilihusika.25/12/2014.



Wasanii wa Hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva,Faridi Kubanda a.k.a Fid Q pamoja na Stamina wakilishambulia jukwaa kwenye tamasha la wazi la Tuo8January,hapo jana katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.

Tuo8January ni kampeni maalum iliyozinduliwa hivi karibuni ikiwa na lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.

Kama vile haitoshi kampeni hiyo inatumika kuwahamasisha vijana wenye uwezo na sifa za kugombea nafasi za uongozi kuchukua hatua sasa za kufanya hivyo,pia kupata vijana wen,vijana wenye vigezo vya kupiga kura pia ni lazima wafanye hivyo maana ni wajibu wetu na kuwa vijana ni lazima tushiriki kikamilifu katika mchakato wa kampeni ili kuhakikisha mambo ya msingi yanajadiliwa na wagombea na yanapewa kipaumbele.

Katika tamasha hilo Fid Q aliwahamasisha vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye tamasha hilo,kuwa imefika wakati wa vijana kujitokeza kushiriki mambo mbalimbali ya kimsingi kwa manufaa ya nchi yao na si kukaa chini na kuanza kulalama,wakati kwenye mambo ya maamuzi wakishirikishwa hawataki kujitokeza,hivyo ni wakati wao wa kuamka na kuchagua kiongozi kijana wa kisasa na si kiongozi wa kisiasa.

Msanii mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.


Baadhi ya wakazi wa mji wa Morogoro wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana kwenye viwanja vya sabasaba mjini humo,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.

Kampeni hiyo ilizinduliwa jijini Dar hivi karibuni na kufanyika tamasha la kwanza mkoani Njombe na sasa Mkoani Morogoro.Baadhi ya Wasanii mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwa vijana wameonesha kuiunga mkono kampeni hiyo,akiwemo Babu Tale, Mwana FA, Nick wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnaba, Ditto,G-nako,Fid Q,Shilole,Yamoto Band,Stamina na wengineo.

Baadhi ya Wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la Tuon8January katika viwanja vya sabasaba mjini Morogoro.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya sabasaba jana jioni mjini Morogoro.

Ilikuwa ni shangwe tu kutoka kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kupitia tamasha la Tuo8January

Mmoja wa wasanii mahiri wa Hip hop,ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya,aitwaye Stamina akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro katika tamasha la Tuo8January,lenye lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.

Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la la Tuo8January,lenye lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.


Baadhi ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana katika viwanja vya Sabasaba,mjini Morogoro.




Pichani kulia ni Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka akiungwa mkono na shabiki wake kwa kunogesha zaidi jukwaa,huku shangwe za mayowe na vifijo zikiwa zimetawala kutoka kwa mashabiki waliofika katika tamasha la Tuo8January hapo jana.

Pichani kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.

watazajamaji wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la Tuo8January hapo jana katika uwanja wa sabasaba mjini Morogoro.

Mkali mwingine wa kufloo freestyle,Godzilla akipanda katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,tayari kwa kuwaburudisha wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.

Diamond Platnumz Afika Ikulu Kwa Kishindo Atimba Kw a Jk akiwa na Tuzo Zake Tano.

Fuatilia hapa zaidi................!

 
Msanii Diamond Platnumz amepata nafasi ya kipekee ya kukutana na rais leo December 23 2014 kwenye Ikulu ya Tanzania. Diamond amekaribishwa ikulu kwenda kupokea shukrani kwa kufanikiwa kuwakilisha taifa la Tanzania vizuri kwenye tuzo tofauti nje na ndani ya africa zikiwemo za kituo kikubwa cha Tv cha Channel O zilizofanyika mwaka huu huko Afrika Kusini.

Diamond Platnumz alikuwenda na tuzo zake tano na kumuonyesha Rais Jakaya Kikwete.



Ijumaa, 12 Desemba 2014

Raisi Jk amtunuku Muuza chips nishani ya ushupavu.


 
Rais Jakaya Kikwete akimvisha Nishani ya Ushupavu Kassim Said Kassim ambaye ni muuza Chips katika maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam, Kassim alitunukiwa Nishani hiyo baada ya kupambana na jambazi aliyevamina na kupora wateja katika eneo la biashara yake na kumpiga chepe na kusababisha kupatikana kwa bastola moja pamoja na risasi tano.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumanne, Desemba 9, 2014 ametunuku Nishani ya Ushupavu kwa mfanyabiashara ya kukaanga na kuuza viazi (chips) wa Dare s Salaam , Bwana Kassim Saidi Kassim, kwa kitendo chake cha kuokoa wananchi dhidi ya jambazi. Bwana Kassim Saidi Kassim alikuwa mmoja wa watunukiwa 28 wa nishani mbali mbali ambazo Rais Kikwete alitunuku ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 53 ya Uhuru. Katika sherehe ya kutunuku nishani iliyofanyika kwenye Bustani za Ikulu Rais Kikwete alieleza kuwa amemtunuku Bwana Kassim Nishani hiyo kwa sababu ya kitendo cha ushupavu alichokionyesha cha kujitoa mhanga kukabiliana na jambazi mwenye silaha ambaye angeleta madhara makubwa. Katika maelezo yaliyosomwa kabla ya Rais Kikwete kumtunuku Nishani hiyo, ilielezwa kuwa mnamo Julai 7, mwaka jana, 2013, majira ya saa 3:15 usiku, Bwana Kassim akiwa katika eneo lake la biashara, alitokea jambazi akiwa na silaha aina ya bastola na kuanza kuwashambulia wateja kwa kuwapiga makofi na kuwapora mali zao na fedha zao. Iliendeleza kuelezwa: “Kwa ushupavu mkubwa ulichukua chepe na kumpiga jambazi huyo mara mbili kichwani, kipigo kilichosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Kitendo hicho kilifanikisha kukamatwa kwa bastola aina ya Glock ambayo nambari zake zilikuwa zimefutwa ikiwa na risasi tano ndani yake na hivyo kuepusha madhara ambayo yangeweza kusababishwa na matumizi mabaya ya silaha hiyo.” Bwana Kassim anakuwa muuza chips wa kwanza katika historia ya Tanzania kutunukiwa Nishani ya Ushapavu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bwana Kassim mwenye umri wa miaka 28 alizaliwa katika Kijiji cha Namwinyu, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma mwaka 1986. Alisoma na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2002 katika Shule ya Msingi ya Ilala, iliyoko Wilaya ya Ilala, Dar Es Salaam. Baada ya kumaliza elimu ya msingi, alianza kujishughulisha na biashara ya kukaaga na kuuza viazi (chips) katika eneo la Buguruni Malapa.

Chid Benz Amshauri Diamond Platnumz Kuyamaliza Kuistaarabu Na Davido .

 Aombe Msamaha Kwa na 

 
Kufuatia Beef la Chini chini kati ya Mwanamuziki Davido na Diamond linaloendelea kwenye Mitandao Baada ya Davido Kudiss Ushindi wa Tanzania Kwenye Shindano la Big Brother Afrika na Diamond Kujibu kiana Kupitia Instagram, Msanii Mkongwe wa Music wa Bongo Flava Ameibuka na Kusema Haya hapa Chini:

Mayweather ATOA USHAHIDI KUPITIA SKYPE JUU YA MAUWAJI YA RAPPER EARL HAYES.

 atoa ushuhuda juu ya rafiki yake kumuua mkewe na kisha kujiuwa mwenyewe

Bondia Floyde Mayweather ametoa ushuhuda wake kwa polisi wa katika interview ya masaa mawili juu ya mauaji yaliyotokea wiki hii pale rafiki na rapper Earl Hayes alipomuua mke wake na kisha kujiua mwenyewe wakati alipokuwa akionge nae kupitia "face time"  ambayo ni kama skype
Floyd amethibitisha kuwa alikuwa akiongea na Hayes (huku wakionana) siku ya jumatatu wakati rapper huyo alipoondoka kwenye simu nakueelekea bafuni na kummiminia risasi kadhaa mke wake, Stephanie Moseley.


Mayweather amewaambia wapelelezi kuwa baada ya Hayes kumpiga risasi mkewe, alirudi kwenye simu na kuendelea kuongea nae na kumwambia anaenda kujiua na yeye  na Mayweather alimuomba asifanye hivyo

Kilichotokea kabla ya mauaji hayo, Floyde amewaambia amesema alikuwa akiongea na Hayes kuhusu mkewe kum-cheat katika mapenzi yao ambapo alidai kuwa alikuwa amejiingiza katika uhusiano wa kimapenxi na muimbaji Trey Songs

alipoulizwa kwanini Hayes alimpigia simu saa moja ya asubuhi, alisema ni kwasababu walikuwa ni marafiki sana na likuwa akijaribu kumuaga.

Idris na Samantha wadaiwa kuwa na mapenzi ya vuguvugu.

Baada ya Jumba la Big Brother AfricaIdris na Samantha ni Kama Penzi Limeanza  .

 
 Waliokuwa washiriki wa mashindano ya Big Brother Africa Hotshots, Idris Sultan wa Tanzania na Samantha Jensen wa South Africa wameanza kuonesha ukaribu wakiwa nje ya jumba la mashindano hayo.

Idris ambaye kwa sasa yuko South Africa Majira ya saa sita na nusu usiku walipost picha wakiwa pamoja kwenye mtoko wao, ikiwa siku moja tangu Idris kuwa akitumia simu na akaunti ya Samantha ya Instagram.
Mara kadhaa Samantha amekuwa akikiri kumpenda Idris. 
Na tangu Idris atoke kwenye jumba hilo Samantha amekuwa akipost kwenye Instagram picha alizopiga akiwa na Idris zaidi.
Wawili waliokuwa wakionesha ukaribu mkubwa wakiwa ndani ya jumba la BBA na baada ya Samatha kutolewa alikuwa akifanya jitihada za kumpigia kampeni za kumuombea kura Idris hadi siku ya mwisho.

NEEMA KWA WATANZANIA HAPPINESS WATIMANYA NDANI YA TOP TEN MISS WORLD.

Miss Tanzania aingia Top Ten Miss Word


 Hii ni baada ya furaha kubwa ya watanzania kwa kuchukua ushindi katika jumba la BBA, Idris ndiye aliyeibuka kuwa mshindi wa dola za kimarekani laki tatu, ni baada tu ya siku kadhaa Diamond kuwa mshindi wa tuzo 3 za Channel O.

Hatimaye  mshiriki wetu kwenye Mashindano ya Miss World ‘Happiness Watimanya’ ambaye ameiwakilisha vizuri Tanzania kwa kuingia kwenye kumi bora za mashindano ya Miss World huku watanzania tukiwa ndio mara ya kwanza kushiriki.

Tizama picha za plutnumz akila bata na watoto baada ya kupokelewa nchini Kenya..!

watoto wafurahia mgeni aje wenyeji wapone hii ni bata batani..!

Diamond plutnum na timu yake ya wasafi wainakshi kenya.

 shangwe kenya  wamkubali tizama mapigo yote hapa waswahili husema nabii hakubali kwao.. 



Hizi ni Stori kubwa muhimu zilizopewa nafasi kwenye Magazeti la leo Tanzania December 12, 2014

UHURU
Umoja wa katiba ya wananchi  Ukawa umevunjika rasmi katika jiji la Arusha baada ya vyama washirika kugomea makubaliano na kila kimoja kusimamisha wagombea.
Awali makubaliano ya Ukawa unaoundwa na vyama vya CUF,NCCR -Mageuzi,NLD na CHADEMA yalifanyika kwa mbwembwe,yalikua washirikiane kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi Urais.
Makubaliano hayo yalitiwa saini katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam ambapo viongozi wakuu wa vyama hivyo walijinadi kuwa watashirikiana na kusimamisha mgombea mmoja katika kila uchaguzi.
Hata hivyo katika jiji la Arusha mambo yameonekana kwenda kombo ambapo vyama hivyo kila mmoja amesimamisha mgombea wake  na kukataa muungano huo huku baadhi yao walikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa muungano wa Ukawa ni kiini macho na hauna tija kwa Watanzania.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Juma Iddi alisema CCM imesimamisha wagombea katika mitaa yote 155 ambapo kati yake mitano wagombea wake wamepita bila kupingwa.
HABARILEO
Katika hali isiyokua ya kawaida mama wa watoto watatu,mkazi wa Wilayani Bunda mwanzoni mwa wiki hii aliamua kuwatelekeza watoto wake wote watatu porini akiwemo wa miezi mitatu wakati wa usiku.
Tukio hilo limethibitishwa na Polisi wanaoendelea kumtafuta mama huyo anayejulikana kwa jina la Wakuru Omar kuhusu ukatili dhidi ya watoto hao.
Msimamizi wa haki za binadamuna watoto katika kata ya salama,L,yidia Kabaka alisemawatoto hao walitelekezwa usiku wa Disemba9 mwaka huu baada yamama hao kutupa watoto hao huku mmoja akiwa ni mchanga mwenye miezi mitatu huku wengine wakiwa na miaka miwili na mitatu.
Alifafanua kuwa mwanamke huyo aliolewa na mumeweambaye alikua na wanawake wengine wawili na alifanikiwa kuzaa naye watoto wanne na mmoja alifariki na yeye kuanza kuwa mlevi wa kupindua na usababisha kuleta ugomvi mkubwa ndani ya familia.
Alisema watoto hao waliokolewa na wapita njiabaada ya kusikia wanalia kutokana na kutaabika kwa kupigwa na baridi pamoja na kuwa na njaa kali.
HABARILEO
Jumla ya Watanzania milioni 11.4 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika jumapili ambao ni sawa na asilimia 62 ya lengo lililowekwa.
Katika uchaguzi huo watakaochaguliwa ni wenyeviti wa vijiji na wajumbe wa kamati za mitaa na wenyeviti wa vitongoji.
Mkoa wa Katavi umeongoza kwa kuandikisha asilimia 78 ya wapigakura huku Dar es salaam umetajwa kufanya vibaya katika kuandikisha wapigakura ambapo waliojiandikisha ni asilimia 43 pekee.
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa katika ofisi ya Waziri mkuu,TAMISEMI Calist Luanda alisema katika uchaguzi huo walitarajia kuandikisha wapigakura 18,587,742 na kusema matarajio hayo yalipatikana kutokana na taarifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka2012 ambayo inaonekana kuwa asilimia10 ya Watanzania wana miaka18 na kuendelea.
MWANANCHI
Wakati Serikali ya Marekani ikisema haitatoa fedha za changamoto za milenia MCC hadi utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow wa bilioni 306 utakapofanyiwa kazi,Ikulu imesema Rais Kikwete hatatekeleza agizo hilo kwa shinikizo la msaada huo.
MCC ni taasisi ya Serikali ya Marekeni inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea na shughuli za MCC zinajengwa katika misingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa zaidi pale tu unapoimarisha utawala bora,uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao wanakuza uchumi na kuondoa umaskini.
Taarifa iliyotolewa na badi ya MCC ilieleza hofu na masikitiko  kuhusu hali ya rushwainavyoendelea hapa nchini.
Fedha ambazo Tanzania litarajia kupata kupitia mradi huo wa MCC awamu ya pili ni dola milioni 450 ambazo ni sawa bilioni765 za kitanzania.
Balozi wa Marekani nchini Mark Childress alisema “Kupigwa hatua katika mapambanodhidi ya rushwa ni muhimu sana kwa mkataba mpaya kati ya MCC na Tanzania na katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara Tanzania”alisema.
MWANANCHI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema ukosefu wa fedha ni moja ya sababu ya kutaka kulitumia jeshi la wananchi JWTZ kusimamia uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapigakura.
Ilisema awali ilitaka kuwatumia walimu lakini baada ya kufuatilia ilielezwa kuwa kipindi ambacho yatafanyika maboresho hayo,itakua vigumu walimu kupatikana.
Mkurugenzi wa NEC  Julius Malaba alisema timu hiyo itasimamia uandikishwaji na kufanya matengenezo madogo madogo ya vifaa wakati wa uandikishaji iwapo yatahitajika.
Hata hivyo mpango huo wa kuwatumia JWTZ umepingwa vikali na vyama vya upinzani wakidai unaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko.
MWANANCHI
Polisi Mkoan Kigoma inamshikilia Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kwa tuhuma za uchochezi.
Kafulila anadaiwa kuwachochea wananchi kugomea kujitolea ujenzi wa Maabara za shule za Sekondari katika jimbo lake.
Taarifa ya kukamatwa kwake ilitolewa jana jiioni na kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jaffar Mohamed na kudai wanamshkilia Mbunge huyo kwa mahojiano zaidi.
Alisema Kafulila alikamatwa jana akiwa katika kata ya Nguruka alikodaiwa kuwa alitoa kauli hiyo ya kichochezi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo ambayo iko jimboni kwake.
MTANZANIA
Simba tisa kutoka hifadhi ya Taifa ya Saadan Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wamevamia makazi ya watu na kushambulia mbuzi sita waliokua katika zizi linalomilikiwa na mkazi wa Kijiji cha Mbwewe aliyetambulika kwa jila moja la Mtongwe.
Akizungumza na Mtanzana jana mkazi wa eneo hilo ambaye alishuhudia tukio hilo Juma Said  alisema huo ni mwendelezi wa uvamizi wa wanyama katika vijiji vilivyopakana na hifadhi hiyo.
“Sasa hivi wakazi wa Saadan tunaishi kwa wasiwasi mkubwa,wanyama wanatoka mbugani wanakuja katika makazi ya watu na tukio la Simba kuvamia mbuzi si jambo la ajabu kwa wakazi wa hapa na baada ya wakazi kutoka na kupiga kelele ndipo wakakimbia”alisema Juma.
Alisema matukio ya wanyama wakali kuingia katika makazi ya watu yamesabababisha kufungwa kwa shule ya msingi Stamico mwezi Oktoba mwaka huu ambapo wanafunzi walikua wakilalamikia hatua ya kuvamiwa na wanyama wakali pindi wanapokua wanaendelea na masomo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Ahmed Kipozi alisema ana taarifa za wanyama kufika katika makazi ya watu na kula mbuzi na tayari askari wa wanyama pori wanafanya uchunguzi ili kujua kiini cha tatizo.

Operator anajikuta akiweka picha za utupu katika bango uwanjani mzigo wa gunia la misumari lamwangukia.

Aseti picha za utupu hadhira washuhudia vioja....

Billboard IIAjali popote, huyu jamaa amepata ajali kazini tena huenda katika mazingira ambayo hakuwahi kutarajia.
Kutokana na sheria kali za China, hii haikuwa makusudi lakini kwa sababu tayari kashafanya kosa anastahili hukumu.
Tumezoea kuona mabango ya kisasa katikati ya Miji kama Dar ambayo yanakuwa yanaonyesha picha kama Tv ambapo picha zinazoonekana kuwa zinabadilika badilika.
Nje ya Uwanja wa Maryland, Langzhou China jamaa anayehusika kuoperate bango moja amejikuta akiwa na hatia ya kukaa jela kwa siku 15 pamoja na na kulipa faini ya kiasi cha Yuan 3000 za China zaidi ya Dola 484 kwa kosa la kuweka picha za wasichana wakiwa tupu kwenye bango lililopo nje ya uwanja huo.
Japo walinzi waliwahi kuchomoa waya wa umeme kulizima bango hilo haikusaidia, watu walioshuhudia picha hizo zikionekana kwa  sekunde 12 walirekodi video na picha ambazo walianza kushare kupitia mitandao ya kijamii.
Mhandisi wa Kampuni inayohusika na kuweka mabango hayo naye pia amekamatwa japo hukumu yake bado haijafahamika.

HII KALI YAO SASA MWANA FA ALKIBA MWANA DAR-ES SALAAM KUFANYA VIDEO ITAKAYO TAMBULIKA KAMA KIBOKO YANGU.

Baada ya kuachia Mfalme hizi ni picha za Mwana FA akiwa katika maandalizi ya video nyingine

.
Ali Kiba akiwa na Warembo katika utengenezaji wa video hiyo mpya ‘Kiboko Yangu aliyoshirikishwa na Mwana FA.
Sina Shaka na wewe mtu wa nguvu utakuwa umeshaisikiliza single mpya ya Hamisi Mwinjuma aka Mwana FA ‘Kiboko Yangu’ aliyomshirikisha Ali Kiba ambayo inaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio.
Good news ninayotaka kukupatia ni kwamba wakati single hiyo ikiendelea kufanya vizuri kwenye spika za radio yako soon inatarajiwa kuona kwenye chati za TV na hizi ndio baadhi ya picha za Behind  The Scene ambazo zikimuonesha Mwana FA na Ali Kiba wakiwa location katika uandaaji wa video hiyo mpya Kiboko Yangu.

.
.
.
.
.
.
.
Ali Kiba na Mwana FA wakiwa Location katika utengenezaji wa video mpya hiyo Kiboko Yangu.
.
Ali Kiba akiwa na Warembo katika utengenezaji wa video hiyo mpya.