UHURU
Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa umevunjika rasmi katika jiji la Arusha baada ya vyama washirika kugomea makubaliano na kila kimoja kusimamisha wagombea.
Awali makubaliano ya Ukawa unaoundwa na vyama vya CUF,NCCR -Mageuzi,NLD na CHADEMA yalifanyika kwa mbwembwe,yalikua washirikiane kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi Urais.
Makubaliano hayo yalitiwa saini katika viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam ambapo viongozi wakuu wa vyama hivyo walijinadi kuwa watashirikiana na kusimamisha mgombea mmoja katika kila uchaguzi.
Hata hivyo katika jiji la Arusha mambo yameonekana kwenda kombo ambapo vyama hivyo kila mmoja amesimamisha mgombea wake na kukataa muungano huo huku baadhi yao walikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa muungano wa Ukawa ni kiini macho na hauna tija kwa Watanzania.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha Juma Iddi alisema CCM imesimamisha wagombea katika mitaa yote 155 ambapo kati yake mitano wagombea wake wamepita bila kupingwa.
HABARILEO
Katika hali isiyokua ya kawaida mama wa watoto watatu,mkazi wa Wilayani Bunda mwanzoni mwa wiki hii aliamua kuwatelekeza watoto wake wote watatu porini akiwemo wa miezi mitatu wakati wa usiku.
Tukio hilo limethibitishwa na Polisi wanaoendelea kumtafuta mama huyo anayejulikana kwa jina la Wakuru Omar kuhusu ukatili dhidi ya watoto hao.
Msimamizi wa haki za binadamuna watoto katika kata ya salama,L,yidia Kabaka alisemawatoto hao walitelekezwa usiku wa Disemba9 mwaka huu baada yamama hao kutupa watoto hao huku mmoja akiwa ni mchanga mwenye miezi mitatu huku wengine wakiwa na miaka miwili na mitatu.
Alifafanua kuwa mwanamke huyo aliolewa na mumeweambaye alikua na wanawake wengine wawili na alifanikiwa kuzaa naye watoto wanne na mmoja alifariki na yeye kuanza kuwa mlevi wa kupindua na usababisha kuleta ugomvi mkubwa ndani ya familia.
Alisema watoto hao waliokolewa na wapita njiabaada ya kusikia wanalia kutokana na kutaabika kwa kupigwa na baridi pamoja na kuwa na njaa kali.
HABARILEO
Jumla ya Watanzania milioni 11.4 wamejiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika jumapili ambao ni sawa na asilimia 62 ya lengo lililowekwa.
Katika uchaguzi huo watakaochaguliwa ni wenyeviti wa vijiji na wajumbe wa kamati za mitaa na wenyeviti wa vitongoji.
Mkoa wa Katavi umeongoza kwa kuandikisha asilimia 78 ya wapigakura huku Dar es salaam umetajwa kufanya vibaya katika kuandikisha wapigakura ambapo waliojiandikisha ni asilimia 43 pekee.
Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa katika ofisi ya Waziri mkuu,TAMISEMI Calist Luanda alisema katika uchaguzi huo walitarajia kuandikisha wapigakura 18,587,742 na kusema matarajio hayo yalipatikana kutokana na taarifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka2012 ambayo inaonekana kuwa asilimia10 ya Watanzania wana miaka18 na kuendelea.
MWANANCHI
Wakati Serikali ya Marekani ikisema haitatoa fedha za changamoto za milenia MCC hadi utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu ufisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow wa bilioni 306 utakapofanyiwa kazi,Ikulu imesema Rais Kikwete hatatekeleza agizo hilo kwa shinikizo la msaada huo.
MCC ni taasisi ya Serikali ya Marekeni inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea na shughuli za MCC zinajengwa katika misingi kwamba msaada utaleta ufanisi na matokeo makubwa zaidi pale tu unapoimarisha utawala bora,uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu ambao wanakuza uchumi na kuondoa umaskini.
Taarifa iliyotolewa na badi ya MCC ilieleza hofu na masikitiko kuhusu hali ya rushwainavyoendelea hapa nchini.
Fedha ambazo Tanzania litarajia kupata kupitia mradi huo wa MCC awamu ya pili ni dola milioni 450 ambazo ni sawa bilioni765 za kitanzania.
Balozi wa Marekani nchini Mark Childress alisema “Kupigwa hatua katika mapambanodhidi ya rushwa ni muhimu sana kwa mkataba mpaya kati ya MCC na Tanzania na katika kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara Tanzania”alisema.
MWANANCHI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema ukosefu wa fedha ni moja ya sababu ya kutaka kulitumia jeshi la wananchi JWTZ kusimamia uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapigakura.
Ilisema awali ilitaka kuwatumia walimu lakini baada ya kufuatilia ilielezwa kuwa kipindi ambacho yatafanyika maboresho hayo,itakua vigumu walimu kupatikana.
Mkurugenzi wa NEC Julius Malaba alisema timu hiyo itasimamia uandikishwaji na kufanya matengenezo madogo madogo ya vifaa wakati wa uandikishaji iwapo yatahitajika.
Hata hivyo mpango huo wa kuwatumia JWTZ umepingwa vikali na vyama vya upinzani wakidai unaweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko.
MWANANCHI
Polisi Mkoan Kigoma inamshikilia Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kwa tuhuma za uchochezi.
Kafulila anadaiwa kuwachochea wananchi kugomea kujitolea ujenzi wa Maabara za shule za Sekondari katika jimbo lake.
Taarifa ya kukamatwa kwake ilitolewa jana jiioni na kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jaffar Mohamed na kudai wanamshkilia Mbunge huyo kwa mahojiano zaidi.
Alisema Kafulila alikamatwa jana akiwa katika kata ya Nguruka alikodaiwa kuwa alitoa kauli hiyo ya kichochezi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo ambayo iko jimboni kwake.
MTANZANIA
Simba tisa kutoka hifadhi ya Taifa ya Saadan Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani wamevamia makazi ya watu na kushambulia mbuzi sita waliokua katika zizi linalomilikiwa na mkazi wa Kijiji cha Mbwewe aliyetambulika kwa jila moja la Mtongwe.
Akizungumza na Mtanzana jana mkazi wa eneo hilo ambaye alishuhudia tukio hilo Juma Said alisema huo ni mwendelezi wa uvamizi wa wanyama katika vijiji vilivyopakana na hifadhi hiyo.
“Sasa hivi wakazi wa Saadan tunaishi kwa wasiwasi mkubwa,wanyama wanatoka mbugani wanakuja katika makazi ya watu na tukio la Simba kuvamia mbuzi si jambo la ajabu kwa wakazi wa hapa na baada ya wakazi kutoka na kupiga kelele ndipo wakakimbia”alisema Juma.
Alisema matukio ya wanyama wakali kuingia katika makazi ya watu yamesabababisha kufungwa kwa shule ya msingi Stamico mwezi Oktoba mwaka huu ambapo wanafunzi walikua wakilalamikia hatua ya kuvamiwa na wanyama wakali pindi wanapokua wanaendelea na masomo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi alisema ana taarifa za wanyama kufika katika makazi ya watu na kula mbuzi na tayari askari wa wanyama pori wanafanya uchunguzi ili kujua kiini cha tatizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni