![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWxWNH8zitK4ToeR61PreblEX7vTq4vzCLCdz-TtNQLtJ_Ahn-3kKZxhom_ZqhmDAGypDJieHznbcmw-c76HZUPegKSf5baTL_1NGhbrtDeqlfEcc_NvesMj3_iRiTZ6YKBiDgQ4c6cCAG/s640/IMG_9341.png)
Ligi kuu ya Uingereza imeendelea hii leo na viongozi wa ligi katika klabu ya Chelsea leo walisafiri hadi katika dimba la St James Park kucheza Newcastle United.
Wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika ligi kuu msimu huu Chelsea leo wamejikuta wakilamba pua na ndoto zao kushindwa kumaliza katika msimu huu bila kufungwa zikipotea.
Hii ni baada ya kupokea kipigo cha 2-1 kutoka Newcastle, timu ambayo Jose Mourinho hajawahi kuifunga katika uwanja wake wa nyumbani tangu alipowasili England kwa mara ya kwanza mpaka leo hii.
Huku magoli ya msenegali Papiss Cisse kulizamisha jahazi la Chelsea ambapo kama itakumbukwa leo waliwezakumkosa mchezaji wao muhimu sana Nemanja Matic.
Kwa uchungu Didier Drogba akiiifungia Chelsea goli la kufutia machozi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni