Taharuki imewakuta wananchi walikuwa
kwenye viwanja vya mahakama Kuu Kanda ya Arusha, wakati polisi wakiwakamata
wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu mara baada ya
mahakama kuwaachia huru.
Muda mfupi baada ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, David Mrango, kumuachia wakili maarufu jijini hapa Median Mwale na wenzake watatu.
Washitakiwa hao ambao waliamua kukimbia huku mmoja, Don Bosco Gichana raia wa Kenya akifanikiwa kuruka uzio WA mahakama na kukamatwa na polisi maeneo karibu na hoteli ya kitalii ya Mount Meru.
Aidha aliyekuwa mshitakiwa, Elias Ndejembi ndiye alikuwa wa kwanza kukamatwa kwani mara baada ya uamuzi huo alitoka nje ya jengo la mahakama ambapo alitokea FFU mmoja na kumshika.
Hali hiyo iliwafanya mawakili kumuuliza askari huyo anamkamata kwa kosa gani na kama anajua uamuzi ulitolewa na mahakama wa kuzuia washitakiwa hao wasikamatwe.
Hata hivyo idadi ya askari wakiongea wakiwemo waliovaa kiraia hivyo kuanza kumvuta mshitakiwa huyo kuelekea kwenye gari ya polisi aina ya Land rover yenye namba za usajili PT 1222.
Mke wa Ndejembi, Imelda aliamua kupigwa picha namna polisi wanavyovutana na mume wake ambapo polisi waliamua kumnyang'anya simu yake na yeye kuanza kulia huku akimng'ang'ania polisi aliyevaa kiraia amrudishie.
Polisi huyo alikerwa na hali hiyo hivyo kuwaagiza polisi kumkamata na kumpakia kwenye gari hilo ambapo askari hao WA kiume walimpandisha kwenye gari hilo hivyo kuwaagiza chini ya ulinzi pamoja na mume wake.
Kwa upande wake wakili Mwale alikamatwa nyuma ya jengo la mahakama ya biashara na kuingizwa kwenye gari aina ya Land Rover yenye namba za usajili T 953 CSZ pamoja na Boniface Mwimbwa.
Magari hayo yaliondoka mahakamani kuelekea kituo kikuu cha polisi.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni