Imeelezwa kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia unasababishwa
na imani potofu za kishirikina zinazochangiwa na matapeli wanaojiita waganga wa
jadi na kujihusisha na ramli chonganishi.
Hayo yamebainishwa na wadau wa ulinzi wa watoto kupitia
dawati la jinsia na watoto nchini Zanzibar katika ziara ya siku tano mkoani
Kilimanjaro katika wilaya ya Hai iliyojumuisha viongozi mbalimbali kutoka nchini
humo kwa lengo la kubaini na kujifunza mbinu mbalimbali katika kukabiliana na
changamoto za kiukatili dhidi ya watoto.
Ukatili wa kijinsia ni tatizo kubwa ambalo linawanyima uhuru
wanaume, wanawake na watoto kufurahia haki zao za msingi ambazo pia ni haki za
binadamu.
Wamesema tatizo hili linaonekana zaidi kwa wanawake kutokana
na hali duni ya kiuchumi na kutofahamu sheria kuongeza idadi ya wahanga wengi
wa ukatili wa kijinsia kimwili, kingono na kisaikolojia.
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu
wizara ya kazi,uwezeshaji wazee,vijana,wanawake na watoto nchini Zanzibar
Hassan Khatibu Hassan amesema vitendo vya ukatili vinasababisha wanawake
kupata maumivu, yanayotokana na vitisho, kunyimwa uhuru mbele ya jumuiya au
eneo la faragha.
Akifafanua zaidi amesema ukatili wa kijinsia umegawanyika
katika makundi mbalimbali ikiwemo
ukatili wa kimwili “ni matendo anayofanyiwa mwanamke au
mwanaume kwa kuumizwa sehemu za mwili wake ikiwemo shambulio la mwili, kukeketa wanawake,
kupiga, kuchoma mwili moto, matumizi ya silaha kwenye mwili, matumizi ya vitu
vyenye ncha kali kudhuru mwili, kuvuta nywele, usukuma, kunyonga mkono au mguu,
kupiga kichwa au kubamizia ukutani”.
Ukatili wa kisaikolojia” Muathirika wa ukatili wa namna hii
hupata maumivu bila watu wengine kutambua kuwa amepata maumivu ambayo humsababishia
mtu maumivu ya kihisia na kiakili
mwathirika kuona amedharauliwa na kushushwa adhi yake katika
jamii kwa sababu tu ya jinsi yake
mfano matusi kwa njia ya ishara au maneno yenye lengo la
kudhalilisha, kutishia kufanya fujo, maneno ya fedheha, dharau au kutishia
kutoa siri hadharani, kunyang’anywa watoto kwa makusudi, kuingiliwa faragha,
kutishiwa kuuawa, kunyang’anywa watoto kwa makusudi, wivu wa kupindukia.
Ukatili wa kingono” ukatili utokanao na mila na desturi
zenye madhara ukatili huu unahusisha masuala ya ngono na mahusiano ya mapenzi
iwe katika ndoa au nje ya ndoa Kwa mfano
matumizi ya vitu kama chuma, fimbo, kisu, mti n.k kuingiza kwenye sehemu
za siri za mwanamke au mwanamume, kubaka, kujaribu kubaka/jaribio la kubaka,
kulawiti (kuingilia kinyume cha maumbile), usafi rishaji/utoroshaji wa binadamu
kwa ajili ya ngono, utumwa wa kingono, unyanyasaji wa kingono, bugudha za
kingono mfano kutomaswa sehemu za matiti, makalio, kiuno na sehemu nyingine za
mwili bila ridhaa, kulazimisha tendo la ndoa hata kama ni wanandoa, ndoa za
utotoni, kupima ubikira kwa wasichana, kulazimisha kutoa mimba, kulazimisha kutia
mimba, kulazimisha ngono bila kujali maambukizi ya magonjwa kama VVU na UKIMWI
na magonjwa mengine ya zinaa na kulazimisha kufanya biashara ya ukahaba.
Aidha Hassan amesema kupitia ukatili wa aina mbalimbali
yamekuwa yakisababisha madhara makubwa katika jamii ikiwemo majeraha, ulemavu
wa kudumu, vifo, huzuni, msongo wa mawazo, kushindwa kutimiza majukumu ya
ulezi, uzazi na uzalishaji, kuharibika kwa mimba, migogoro kwenye familia,kushuka
kwa uchumi kutokana na mzigo mkubwa kwenye huduma za afya ya
Umma na kupungua kwa uzalishaji malina hatimaye kulegalega
kwa malezi ya watoto.
TIZAMA PICHA MUHIMU KATIKA TUKIO HILI.