![]() |
Wito umetolewa kwa Wanawake wajasiriamali mkoani Kilimanjaro kutumia fursa zilizopo ikiwemo kutekeleza kwa vitendo taratibu,kanuni na sheria zilizokwa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira kufuatia ufunguzi
wa kikao cha wanawake wajasiria mali na wafanyabiashara mkoani hapa kilicholenga
kuimarisha mahusiano,kubadilishana ujuzi na kuunda mtandao wa kibiashara katika
ustawi wa uchumi, familia na taifa kwa ujumla.
Mghwira
amesema katika ustawi wa viwanda wanawake wanashiriki asilimia kubwa kuhakikisha
huduma muhimu za kijamii zinapatikana na kuongeza chachu ya ushindani unaozaa matunda katika kukuza uchumi ikiwemo kuimarisha mahusiano miongoni mwa mtu binanfsi ,vikundi,makampuni
na taasisi mbalimbali .
Akifafanua
zaidi amesema dhamira na kipau mbele cha
Mhe. Rais John Pombe Magufuli kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda ,wajasiriamali
wanapaswa kuviwezesha viwanda vidogovidogo vikue katika ustawi mzuri kwa kuzingatia upatikanaji
wa mali ghafi na soko la uhakika .
” Serikali
inawategemea sana ninyi wajasiriamali katika kutekeleza kauli mbiu hii ya
mheshimiwa rais katika kubadilika
kifikra, kuwa na uthubutu na hatimaye kukuza uchumi wa nchi yetu ,Sisi kama
mkoa na Serikali kwa ujumla tutaendelea kushirikiana na sekta binafsi
kuhakikisha kunakuepo na mazingira bora na rafiki kwa wajasiriamali katika mkoa wetu. ” alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Katika
hatua hiyo Mhe. Mghwira
amezitaka taasisi za kifedha kuboresha mikopo nafuu kwa
wajasiriamali wadogowadogo kwa kuzingatia uhalisia wa biashara zao na marejesho
sambamba na mamlaka husika kuwa
waadilifu na kuepuka mianya ya rushwa .
Wakati
huohuo Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wafanyabiashara(TWCC)mkoani hapa
Bi.Joyce Ndosi amesema wanafanya jitihada mbalimbali kuzikamilisha ndoto za wanawake
wajasiriamali kuimarika kiuchumi na
kijamii licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa bidhaa
nje ya mipaka ya nchi na upatikaji wa masoko .
“Mwanamke
ni nguzo ya familia hivyo kujituma na kujishughulisha na biashara ni msingi wa
ustawi wetu katika kuhakikisha familia zetu pamoja na jamiii inakuwa salama, hivyo
TWCC ni jukumu letu kupaza sauti na kuongeza hamasa kwa wanawake kutokua
tegemezi na kupata wigo mpana katika uwajibikaji sambamba na kuzifanya
changamoto kuwa fursa kuzichangamkia fursa katika kukuza uchumi wa nchi.” alisema Ndosi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni