![]() | |||
Pichani ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Eng.Stella Manyanya |
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Stella Manyanya amesema serikali kupitia
wizara yake itatumia busara kumaliza mgogoro uliopo kati ya Mamlaka ya Reli hapa
nchini (Rahco) na kiwanda cha Serengeti Breweries (SBL) kuhusu kubomolewa nusu
ya eneo la kiwanda hicho.
Akizungumza wakati wa ziara yake
fupi ya siku moja mkoani Kilimanjaro iliyolenga
kutembelea viwanda vilivyobinafsishwa na
Serikali ambapo aliambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda ,Biashara na Mazingira iliyolenga kubaini uhalisia wa mgogoro baina
ya Shirika hilo na kiwanda hicho.
Manyanya amesema Serikali inatambua
mchango mkubwa unaofanywa na wawekezaji
haowa SBL kupitia sekta ya viwanda ikiwemo kuongeza pato la taifa sambamba na
kuitangaza Tanzania katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Utalii wa ndani na nje .
“Jina la kiwanda hiki ni sehemu moja
wapo ya kuitangaza Tanzania kwa upande wa utalii kupia mbuga yetu ya wanyama Serengeti, SBL wamekua ni wadau wazuri
baada ya kubinafsishwa, ni walipa kodi wazuri na waaminifu kwa Serikali yetu na
niwapili kwa sasa kiukubwa kwa utoaji wa huduma ya vinywaji aina ya pombe hivyo
tunafurahi kuona baadhi ya viwanda
tulivyovibinafsisha kikiwemo kiwanda hiki vinaendelea vizuri zaidi hususani
katika swala zima la usafi katika ngazi
ya kimataifa”
Amesema uwekezaji uliofanywa katika kiwanda
hicho una tija kubwa kwa wananchi katika ustawi wa uchumi kama ilivyo azma ya
Serikali yetu hivyo kupitia ziara hii tumekutana na changamoto ya mgogoro wa
ardhi baina ya Mamlaka ya reli hapa
nchini na kiwanda hicho ambapo kimsingi
reli hiyo bado haijajengwa.
“Ardhi ipo ya kutosha ,hivyo tutakaa
nawizara zote zinazohusika na jambo hii na kupata suluhu,najua hili halina
tatizo, nipende kuwatoa shaka wawekezaji wetu busara itatumika na mambo
yatakwenda vizuri.Huyu mwekezaji yuko ‘Serious’tunapenda kuona anaendelea
kuwepo hivyo nchi hii ipo kwa ajili ya kuangalia maslahi mapana na mchango
unaofanywa na wawekezaji hawa,”amesema
Manyanya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati
ya Bunge ,Viwanda ,Biashara na Mazingira,Suleiman Sadiki ambaye pia ni Mbunge
wa Mvomero amesema mgogoro huo unahitaji suluhu ya haraka zaidi kwasababu
unashirikisha wawekezaji wawili akiwemo wa ndani na nje ya nchi.
“Wawekezaji hawa tunawakatisha tama kwa
namna moja au nyingine na nia ya kamati hii ya Bunge ni kuunga mkono juhudi mbalimbali za Rais
katika kuelekea Tanzania ya Viwanda ,Tumekutana na changamoto hii ya mgogororo
wa ardhi ambapo tumekutana na mambo makuu matatu moja Uwepo wa kesi iliyopo
Mahakamani,pili Barua ya kubomoa ukuta na tatu ni Kutokuwepo kwa barua
inayoonyesha kuwa mgogoro huo umeisha hivyo kama kamati tumeyabeba haya yote
tunakwenda nayo, kazi yetu kubwa ni
kuishauri Serikali katika ustawi wa viwanda ili tuangalie namna ya kulimaliza
jambo hili kwa haraka kwasababu miongoni mwa viwanda vinavyochangia pato la taifa
kwa kulipa kodi ni Kiwanda hiki cha Serengeti Brewieris “alisema Sadick.
Akifafanua zaidi amesema kupitia
nyaraka mbalimbali za hati za kiwanja hicho zilizopo wataishauri vyema serikali
kuumaliza mgogoro huo mapema iwezekanavyo bila ya kuathiri uhusiano wa
kibiashara kwani enoo la reli mpaka
kufikia kuta za kiwanda hicho lina
ukubwa wa kilometa moja”Wawekezaji hawa wametuambia wana hati mbili ikiwemo ya
eneo lenye mgogoro huo lakini tulipowauliza wenzetu wa Rahco wamesema hawana
hati ya eneo hilo”alisema Sadick.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Mawasiliano SBL John Wanyancha amesema wanaishukuru Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia Kamati hiyo ya Bunge kwa kuipa kipau mbele
sekta ya viwanda hivyo wanaiomba Serikali kuhakikisha eneo hilo halibomolewi
kutokana na uhitaji mkubwa wenye tija kwa wananchi ikiwemo ajira kwa wazawa
,fursa kwa wakulima mbalimbali wakiwemo wa zao la Mahindi,Shairi na Mtama.
FUATILIA TUKIO HILI HAPA BILA KUKOSA.
Pichani aliyetangulia mbele kabisa ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali kiwandani hapo. |
Aliyetangulia mbele ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akiwa ameambatana na Timu ya Kamati ya Bunge na Viongozi mbalimbali wa Serikali. |
Hapa ni ndani ya kiwanda cha Serengeti Bweries (Moshi) Wajumbe wanatembelea kuona hali halisi. |
Hii ni moja ya alama iliyopo mbele kabisa ya kiwanda hicho. |
Aliyenyoosha mkono ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Bw.John Wanyancha akiwaonyenya wajumbe wa kamati ya Bunge na Viongozi juu ya eneo linalodaiwa kuwa litabomolewa kupisha ujenzi wa reli . |
Hapa ni nje ya kiwanda cha SBL-Moshi na hii ni barabara kuu ya Moshi -TPC hatua chache tu kutoka kwenye geti la kiwanda hicho. |
Wajumbe wa Kamati ya Bunge Viwanda,Biashara na Mazingira wakijadiliana kidogo baada ya kuona uhalisia eneo husika n a thani ya Miundombinu. |