| KULIA NI MWENYEKITI WA CCM MKOA WA KILIMANJARO BW.PATRICK BOISAFI ALIYESHIKA KIPAZA SAUTI NI MKUU WAMKOA WA KILIMANJARO DKT.ANNA MGHWIRA ANAYEFUATA NI KATIBU TAWALA MKOA ENG.AISHA AMOUR. |
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna
Mghwira amezitaka Mamlaka husika zinazoshughulikia uhuwishwaji wa taarifa
muhimu za kiutendaji kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuepuka migogoro isiyo
na tija baina yao na walaji sambamba na kuchukua hatua stahiki katika
kutoa huduma za kiada na ziada.
Rai hiyo imetolewa kufuatia mkutano
maalumu wa Wafanya biashara mkoani humo uliolenga kuchakata na kutatua
kero mbalimbali na fursa zinazopatikana ndani ya mkoa katika kukuza
uchumi na ustawi wa biashara .
Mghwira amesema ni vyema taasisi za
Umma zilizopewa dhamana kujitathimini kwa kina ili kuyafikia malengo
yaliyokusudiwa katika kuboresha mfumo wa utoaji huduma muhimu
zilizokusudiwa na kuondoa dhana hafifu zinazo ambatanishwa na itikadi za kisiasa
kupitia kada mbalimbali kwa baadhi ya wananchi juu ya utendaji wa
Serikali yao. “Wafanyabiashara wanailalamikia Mamlaka ya Mapato TRA kwa
kuwanyanyasa na wakati mwingine kuahidi kuzisimamisha huduma mbalimbali pasipo
kuzingatia misingi ya haki , mazingira,wajibu kinga ya kisheria na
kuwakandamiza wafanyabiashara kulipa faini mbalimbali tofauti na dhamana
walizopewa kuelimisha wadau juu ya huduma mbalimbali na jinsi ya kutatua
changamoto zinazowakabili Serikali inafuata misingi sahihi ya uwajibishaji wa
waalifu pasipo kujali itikadi za vyama wala dini ”alisema Mghwira.
Akipokea moja ya hoja kutoka
kwa wafanyabiashara wanaotekeleza wajibu wao katika Stendi kuu ya Mabasi Moshi
wawekezaji hao wameilalamikia Halimashauri ya Manispaa ya Moshi
kupandisha kodi ya vibanda kutoka sh.30,000 kwa mwezi hadi kufikia Sh.400,000
mara baada ya mkataba wa uwekezaji kuisha mnamo 31/12/2018.
Wakifafanua zaidi wawekezaji hao
wamesema tozo hiyo ni kubwa hivyo inawaumiza waliowengi na kuonekana
kutotambulika kwa jitihada walizozionyesha kuiunga mkono Serikali
katika ujenzi wa vibanda hivyo ambapo awali waliwekeza katika jengo
hilo na kuchangia ujenzi wa Sh.4.5Milioni .
Akijibu hoja hiyo Mghwira amesema
hatokubali Serikali ipakwe tope kutokana na uamuzi huo wa Manispaa kwani
kwa kufanya hivyo ni kuonyesha dhahiri kuwa Serikali imeshindwa kutambua na
kuthamini mchango na uwepo wa wafanyabiashara hao .
“Hii kodi mliyoiweka ni kubwa
mno ,mmeenda mbali kwa kutoza kodi kwa kiwango hiki ,mnachokifanya
mnajenga hoja ,mnataka kusema Serikali imeshindwa kutothamini michango ya
wafanya biashara hawa waliojitoa miaka 15 iliyopita kuchangia ujenzi wa jengo
lile, ikumbukwe mtu aliyechangia ujenzi ni tofauti na mtu anayekuja na
dau kubwa ambaye hajachangia ujenzi wa miundo mbinu yoyote” amesema Mghwira.
Hata hivyo Ameitaka
Manispaa ya Moshi kupitia Mstahiki Meya Raymond Mboya na Mkurugenzi
Bw.Michael Mwandezi kutathimini na kuziangalia baadhi ya huduma
zinazolalamikiwa na wawakezaji hao katika eneo la Stendi Kuu ya Moshi
ikiwemo tozo kubwa la pango hali inayosababisha kudhorota kwa
hali ya kibiashara na huduma hafifu kwa walaji.
“ Mbali na kuwepo kwa mgogoro
unaoendelea katika jengo hilo kwa miaka mingi hivi sasa naiagiza Manispaa
ya Moshi kukaa meza moja na wafanyabiashara ili kutatua mgogoro huu
mapema iwezekanavyo sambamba na kupanga viwango vipya vya
kodi,fuateni vigezo na viwango vilivyopo sokoni,soko hili ni huria sio holela
,wekeni bei ambayo haitawaumiza wafanyabiashara hawa wanamchango mkubwa
sana katika jengo lile ”amesema Mghwira.
TIZAMA PICHA ZA MNATO KATIKA
TUKIO HILO.
PICHANI
NI MKURUGENZI WA KAMPUNI YA CHRISBURGER BW.CHRIS SHAYO AKICHANGIA HOJA
KATIKA MKUTANO HUO.
|
PICHANI
NI MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA MOSHI BW.RAYMOND MBOYA AKIJIBU HOJA.
|
|
PICHANI NI KAMANDA
WA UHAMIAJI MKOA WA KILIMANJARO BW.ALBERT RWELAMILA AKIJIBU HOJA.
|
WA
KWANZA KABISA PICHANI ALIYEVAA MIWANI NI AFISA UHUSIANO WA KIWANDA CHA SUKARI TPC-MOSHI BW.JAFARY
MICHAEL.
|
| PICHANI NI MAAFISA WA CRDB BENKI BW.LUDOVICK NGOWI NA ADAM MGAZA WAKIFATILIA HOJA KWA MAKINI. |
| PICHANI NI WADAU WAKIFUATILIA HOJA MBALIMBALI KATIKA MKUTANO HUO. |
| PICHANI NI MWENYEKITI WA DALADALA MANISPAA YA MOSHI BW.SAIDI SELEMANI AKICHANGIA HOJA KUHUSIANA NA SUMATRA. |
MUWAKILISHI
KUTOKA TAASISI YA OSHA BI.WINNIE KIWELU
AKITOA HOJA KATIKA MKUTANO HUO.
|
| PICHANI NI BAADHI YA WADAU WAKISIKILIZA HOJA KWA MAKINI KATIKA MKUTANO HUO. |
WA
KWANZA PICHANI MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HARSHO GROUP BW.HAROLD SHOO ANAYEFUATIA NI MKURUGENZI WA DEMA CONSTRUCTION BW.DISMAS
MASALU ALIMAARUFU (DEDE)
|
PICHANI
NI AFISA WA SIDO BI .LILIAN MATERU AKIJIBU HOJA ZA WAJASIRIAMALI.
|
| WAWAKILISHI KUTOKA NMB BENKI WAKIFUATILIA HOJA KWA MAKINI. |
PICHANI NI MKURUGENZI WA KAMPUNI YA DORKIA ENTERPRRISES BI. DORCAS KIBONA AKITOA HOJA KUHUSIANA NA SIDO. |
PICHANI NI MKURUGENZI
WA MANISPAA YA MOSHI BW.MICHAEL MWANDEZI AKIJIBU HOJA.
|
PICHANI
NI MJUMBE THOMAS MAKYAO AKICHANGIA JAMBO.
|