Mkuu wa Mkoa Wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mgwhira Akizungumza Katika Mkutano Wa Hadhara Uliofanyika Katika Kijiji cha Sanya Station kilichopo Wilayani Hai na Kinachopakana na Uwanja wa Ndega Kia. |
Serikali mkoani Kilimanjaro imeagiza uchunguzi ufanyike dhidi ya askari polisi wanaodaiwa kuwanyanyasa
na kuwatesa wananchi wanaoishi katika kijiji cha Sanya Station kinachopakana na
uwanja wa ndege wa Kia Wilayani Hai.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani humo wanakijiji hao
wameeleza kunyanyaswa ikiwemo
kutumbukizwa kwenye maji machafu ,kutukanwa na kubaguliwa na askari hao sambamba na
kuwafyetulia risasi sizizo na tija katika maeneo wanayoishi na kuhatarisha maisha yao .
Wakifafanua zaidi wamesema wamekuwa wakikamatwa na mifugo yao,kufedheheshwa na kuwekwa chini
ya ulizi basipo sababu za msingi na kutakikana kutoa rushwa ya pesa tasilimu ili kuachiwa huru au kufunguliwa kesi
ambazo zinazowagharimu kutumia muda wao mwingi kuhudhuria Mahakamani na
kushindwa kuendesha shughuli za uzalishaji.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mgwhira
ameeleza kusikikitishwa na baadhi ya watumishi wa jeshi la polisi kuwanyanyasa
wananchi na kuagiza askari hao
watambuliwe na kuchukuliwa hatua kali za
kisheria .
Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoani humo Bw.Hamisi
Issa amesema hayupo tayari kuona wananchi wanafedheheshwa na kufanyiwa vitendo
vya kikatili na askari wanaodaiwa kutenda tukio hilo na kuahidi kuwatambua
askari waliohusika haraka iwezekanavyo na hatua zaidi za kisheria kufuata
mkondo wake.
Katika Picha Ni Wanakijiji wa Sanya Station Wakiwasikiliza Viongozi mbalimbali Waliofika Katika Mkutano huo. |
Pichani Ni Mwenyekiti wa Kijiji Cha Sanya Station Akitoa ufafanuzi Juu Ya Wananchi Wake Wanavyopata Adha Kutoka . |
Katika Picha Ni Mkuu Wa Wilaya Ya Hai Mhe.Lengai Ole SabayaAkitoa Maelezo Ya Kina Juu Ya Mgogoro Huo. |