Pichani ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe |
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewataka
Watanzania kutogombanishwa na baadhi ya kauli za viongozi zisizonatija na
kuleta mipasuko katika jamii husani katika itikadi za kikabila na
kidini huku akiwataka viongozi kutafakari maneno wanayoyateta kwani yanaweza
kugawa watu na kuleta machafuko katika jamii.
Aidha,
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, amemuelezea aliyekuwa Mwenyekiti wa
Kampuni za IPP, Dk. Reginald Mengi alikuwa ni mtu asiyekata tamaa,asiyejivuna
na mwenye busara kwa kila mtu hata wale masikini wa chini kabisa aliwapa
heshima licha ya kuwa alikua tajiri.
Mbowe
ameyasema hayo Punde tu wakati akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya
kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni tanzu za IPP, Dk. Reginald
Mengi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.
“Kuna
kauli zinasemwa sana na watu kwa ukweli zinakera kwa vile mimi Mbowe si mnafiki
lazima niseme na nitasema hapa hapa mbele za watu kwa lengo lakuimarisha utaifa
na sio itikadi za chama,udini au ukabila".
“Tuna
nchi moja ambayo tunastahili kupendana na kusaidiana, na kila mtu ana haki ya
kumsaidia mwenzie, tusikubali kauli za viongozi zitugawe hasa za kidini
na kikabila, kauli ya kusema kuna makabila hayawezi kuwasaidia walemavu si
nzuri na haikutupendeza kwa kweli, tujitafakari tunapotaka kuongea maneno ,”
amesema Mbowe.
Aidha
Mbowe ametoa wito kwa kila aliyeguswa na msiba wa Dk. Mengi kuyaenzi yale yate
aliyokuwa akiyatenda enzi za uhai wake kwani hiyo ndiyo alama pekee
aliyoyuachia na hatuna budi kumuenzi.
“Mzee
Mengi ameshatangulia mbele za haki haitajalisha tuzungumze mema kiasi gani
kumuhusu hatutamrejesha, ila tujitafakari na kuyaenzi yale aliyokuwa
akiyafanya, alikuwa mnyeyekevu na kauli zake zilijenga, kupatanisha na kuleta
matumaini lakini pia hakuwahi kukata tamaa,” amesema Mbowe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni