Waziri
mkuu wa Tanzania Kasimu Majaaliwa, ameongoza maelfu ya watanzania katika
mazishi ya aliyekuwa mfanyabiashara maarufu ukanda wa Afrika mashariki,
Dr. Regnald Mengi, ambaye amezikwa leo katika makaburi ya familia nyumbani kwa
wazazi wake kijiji cha Kisereni Machame mkoani Kilimanjaro Km 35 kutoka Moshi
mjini.
Akitoa salamu
za rambi rambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Waziri
Mkuu Kassim Majaaliwa amesema kuwa taifa litamkumbuka Dkt. Mengi kwa mchango
wake mkubwa wa kukuza uchumi nchini hasa katika sekta ya madini, habari,
viwanda na mazingira, kwani amewahi kuwa mwenyekiti wa abaraza la mazingira
Taifa.
Waziri
mkuu Majaaliwa amesema mchango wa Dkt.Mengi katika kuwakumbuka watu wenye
mahitaji maalumu utaendelea kukumbukwa daima kuindokewa na mtu mzalendo katika
historia ya Tanzania
"Hakuna
Mtanzania asiyejua mchango alioutoa kwa Taifa hili,kwa namna alivyoguswa katika
nyanja mbalimbali kwa jamii na hata kwa serikali, tunatambua mchango
wake"alisema Majaliwa.
Amesema
kuwa kama Taifa la Tanzania msiba huo wa Dkt Reginald Mengi alikuwa ni
mtu wa upendo na hakuwa na ubaguzi hivyo pigo na wameondokewa na mtu aliyekuwa
muhimu maishani na Mungu alimbariki na yeye akawa baraka kwa wengine.
Akitoa
mahubiri katika ibada ya mazishi hayo iliyofanyika katika kanisa la Kiinjili la
Kilutheli Tanzania KKKT Usharika wa Moshi mjini, Askofu mkuu wa Kanisa hilo
Dkt. Fredrick Shoo, amewaasa viongozi wa serikali hasa wale wenye umri mdogo
kuacha kiburi cha madaraka na badala yake watende haki kwa wananchi wote bila
upendeleo na watapata za Mungu.
Dkt Shoo
amemtaja Marehemu Mengi kuwa hakuwabagua maskini japo alikuwa na tajiri
na tabia hiyo inapaswa kuigwa na watu wote wenye nafasi za uongozi serikalini,
wenye madaraka na wenye pesa.
Askofu
Dkt. Shoo asisitiza kuwa kama Taifa la Tanzania linahitaji kupokea baraka
kutoka kwa Mungu ni muhimu kuacha ubaguzi, kiburi na
kujikweza,amekemea baadhi ya tabia ya kauli za viongozi ambazo zinaweza kuleta
migogoro katika jamii.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania Freeman Mbowe,
amekemea tabia ya ubaguzi wa ukabila unaooneshwa na baadhi ya viongozi na
kwamba ili kumuenzi Mengi ni muhimu kuyaacha matendo hayo kwani alikuwa ni mtu
wa kujishusha japo alikuwa Bilionea.
Katika
hatua nyingine Askofu Dkt.Shoo amewataka Watanzania kuacha tabia ya kubaguana
kwani ni dhambi mbele za Mungu ,wenye nafasi kuwakandamiza wale walio wa hali
ya chini,amewataka kuacha kiburi
"Hivi
nyie viongozi haswa vijana mnapopata cheo mnajisahau wanaojitutumua kama chatu
wakumbuke kuwa kila siku tunamuomba Mungu na lazima Mungu
atawashusaha"
Kwa
upande wake Waziri mkuu Kassimu Majaliwa ametoa pole kwa familia ya Marehemu
Dkt.Regnald Mengi kwa kuondokewa na mpendwa wao,amesema amepokea kwa mshtuko
mkubwa taarifa ya msiba wa Mengi
Tujifunze
kuwathamini watu wasio na uwezo katika jamii na Taifa kwa ujumla msikivu
,mpenda amani,na mwenye kuwasaidia wengine 1990 alianza kupata chakula cha
pamoja na watu wenye ulemavu.
Kwa
upande wake Mkuu CCM Taifa Bashiru Ally amesema mchango wa Dkt. Mengi katika
Taifa haswa katika mazingira alisisitiza kupanda na kuotesha mingi
tumuenzi na kupanda miti ya kutosha
"Baba
Askofu hatujafanya kazi ya kuwaandaa vijana wetu kuwa Viongozi bora, sasa
tunavuna matunda yake, naomba nimuombe msamaha kijana wangu Makonda, nilimsema
Simiyu mara ya kwanza, akaja ofisini analia, ameanza kujirekebisha"
alisema Bashiru
Akitoa
salamu kwa niaba ya Bunge Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amesema kuwa
ameonyesha kwa hali na mali alikuwa na mali ila mkarimu na amefanya mengi ya
heshima kubwa,alijitoa bila kujali alipanda miti zaidi ya milioni ishirini siyo
jambo la kawaida.
"Nawaomba
wananchi wenzangu msiamini kila kitu kinachoandikwa kwenye mitandao ya
kijamii ,vingine vya uongo sana.amesema Ndugai
Kwa zaidi
ya mzee mwenzangu ameshatangulia mbele za haki haitajalisha tutazungumza maneno
mazuri kiasi gani ,tutakachowezakukifanya sasa ni kuyaishia kuyaenzi mema aliyotenda,alikuwa
mnyenyekevu,kauli zake zilikuwa za kujenga,kupatanisha,mamlaka,fedha zinajenga
kiburi zisipotumika vizuri,hakuwa kiongozi wa serikali .
Dkt. Mengi amezikwa katika kijiji cha Kisereni Machame mkoani Kilimanjaro,
eneo la makaburi ya familia walipozikwa wazazi wake na ndugu wengi.
TIZAMA HAPA PICHA ZOTE KATIKA TUKIO HILO KUANZIA WAZIRI MKUU AKIPOKELEWA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA KIA AIRPOT.
TIZAMA HAPA PICHA ZOTE KATIKA TUKIO HILO KUANZIA WAZIRI MKUU AKIPOKELEWA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA KIA AIRPOT.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni