Tafuta katika Blogu Hii

Jumamosi, 4 Mei 2019

POLISI TANZANIA YAIBUKA KIDEDEA 2-1DHIDI YA BOMA FC YAFUZU KUELEKEA LIGI KUU.

Hiki ni kikosi cha Polisi Tanzania Fc wakiongozwa na Captain Henerico.
Timu ya Polisi Tanzania imeibuka kidedea na kufuzu kushiriki ligi kuu daraja la kwanza   Tanzania bara mara baada ya kuitandika Bora Fc bao 2-1.
Kikosi cha Polisi Tanzania kikiwa chini ya Captain Henerico Kayombo wameweza kujichukulia pointi tatu kibindoni na kuifanya safari kuwa nyepesi ya kuelekea ligi kuu  Tanzania bara hapo badae.
Mabao hayo yamefungwa namchezaji nguli  jezi nambari 4 mgongoni Patrick Athanas  na kuwainua  mashabiki katika  viti kwa kukonga nyoyo zao huku ushangiliaji wa aina yake ukishika hatamu.
Kikosi hicho  cha Polisi Fc kiliongozwa na   wachezaji  Abdulikarim Segeja,Kurwa  Manzi,Mohamed Kassim,Patrick Athanas,Hassan Kapona,Henerico Kayombo ,Bantu Admin,Juma Ramadhan,Charles Ndahaze,Santos Marcelino na Shaban Stambuli.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Afisa habari wa timu hiyo Bw.Frank Geofray amesema ushindi huo ni sehemu muhimu kwao na kati ya mafanikio yanayosadifu umuhimu wa timu hiyo kwani walikua wanatambua wanachokifanya sambamba na kushukuru uongozi mzima wa timu hiyo katika kuwawezesha kwa hali na mali kuyafikia mafanikio hayo.
 HAPA NI KABLA YA MCHEZO MAANDALIZI NA MORALI ZINAONEKANA ZAIDI KWA   WACHEZAJI NA MASHABIKI.




Hawa ndio Boma Fc ya Mbeya.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issa akiwa amewasili kabla ya mechi kuanza ili kushuhudia mtanange huo.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Dkt.Anna Mgwhira akiwa tayari kufuatilia mechi hiyo.
TIZAMA HAPA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO DR.ANNA MGWHIRA AKISALIMIANA NA WACHEZAJI KABLA YA MECHI HIYO KUANZA.




           HAYA NDIO MAGOLI YA POLISITANZANIA FC DHIDI YA BOMA FC YA MBEYA.

Patrick Athanas anafunga bao la pili na kuwainua mashabiki wa Polisi Tanzania kwenye Majukwaa.
Kamanda wa Polisi Hamisi Issa akiwa na Furaha mara baada ya Polisi Tanzania Fc kupata bao la pili.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr.Anna Mgwhira  akifuatilia kwa makini mtanange huo.
Kamanda Issa akishauriana jambo  na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mwisho kabisa upande wa kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Bw. Bwai Biseko .
Kamanda Issa akishauriana jambo  na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mwisho kabisa upande wa kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Bw. Bwai Biseko .
Kamanda Issa akishauriana jambo  na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mwisho kabisa upande wa kushoto ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Bw. Bwai Biseko .
Dr.Mgwhira akistaajabu jambo la kimichezo mara baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Katibu Tawala wa mkoa Bw.Bwai Biseko.
Picha zifuatazo ni Kocha kiongozi wa timu ya Polisi Tanzania Pamoja na jopo lake akitoa maelekezo kwa wachezaji wake  mara baada ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Mlinda mlango wa timu ya Polisi Tanzania Fc Abdulkarim Segeja akijizatiti kukamilisha Ng'we ya pili katika chezo huo.
Wachezaji wakijizatiti kuukabili mpira katika kipindi cha pili.
Mmoja wa washabiki wa timu ya Polisi Tanzania Fc Akishangilia na kujipongeza mara tu ya Refarii kupuliza kipenga cha Mwisho.