Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 2 Julai 2019

VIJANA ZAIDI YA 60 WAMEDHAMIRIA KUJIKWAMUA KIMAISHA KUPITIA NGUVU KAZI .

Wanakikundi hao wakiwa katika ubora wao.

Vijana zaidi 60 mkoani  Kilimanjaro wameamua kuungana kwa pamoja na kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi ikiwemo ufugaji wa kuku.
Akifafanua zaidi mara baada ya kikao kilicholenga kuchambua na kuipitisha katiba ya kikundi hicho ,Mwenyekiti wa kikundi hicho kijulikanacho kama  Boisafi Coffee Group  (BCG), Willy  Kutika, amesema lengo la kikundi  hicho ni kuhakikisha kila mwanachama ananufaika na umoja waliouunda kwa kusaidiana kwenye shida na raha na kwamba miongoni mwa miradi ambayo wamekusudia kuifanya ni ufugaji wa kuku,mbuzi,ng’ombe,biashara ndogondogo pamoja na kilimo ili kukuza uchumi wa kikundi hicho.
“Ili tuweze kwenda sambamba kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi zinavyoelekeza nasisi leo tumeunda katiba itakayokiongoza kikundi chetu kwa kanuni,na hii nikutekeleza dhumuni la umoja ,upendo na mshikamano ili kupata maendeleo yenye tija kwa kila mmoja watu”alisema Kutika.
Katika hatua hiyo amesema “Kikundi hiki kimeanzishwa mwaka huu (2019) kikiwa na wananchama 30 ambapo baadae waliogezeka na kufikia 64 kwa kuhamasishana sisi kwa sisi ili tuondokane na umasikini kwenye  jamii zetu na taifa kwa ujumla ,pia kwa sasa kuna mwanakikundi mwenzetu mgonjwa ambaye tunaendelea kumsaidia kwa umoja wetu.”Alisema Willy
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya vijana hao ambao miongoni mwao ni wakereketwa wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani hapa wamesema kwa umoja huo utawafanya kufikia malengo waliyojiwekea kwani katiba hiyo itawapa hari na chachu  kwa mwanakikundi kufuata taratibu zilizowekwa.
 .“Kikundi hetu hiki tangu nimejiunga nimepata mabadiliko makubwa kiuchumi kwa kupiga hatua kutokan na umoja wa wenzangu,mawazo na ushauri ninaopata umenisaidia,pia hii ni  ishara mojawapo ya kuunga mkono jitihada za raisi wetu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dr.John Pombe Magufuli za kukuza maendeleo ya nchi.”alisema Alex Mtondo  mwanacham wa kikundi hicho
 “Kwasasa vijana wengi wamejiunga kwenye vikundi vinavyowanufaisha na kuendeleza malengo yao,ili muendelee kunufaika kwenye vikundi hivi hakikisheni mnajisajili kama vikundi vya biashara kama kilivyo hiki chenu cha Boisafi Coffee Group (CBGs), hii itawafanya kuwa na sifa ya kupata mikopo mbalimbali inayotolewa kwenye halamshauri nchini.”Alisema Kheri James ambaye ni Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi  Taifa (UVCCM) wakati alipokua akizindua kikundi hicho june 15 mwaka huu mkoani hapa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni