Tafuta katika Blogu Hii
Jumamosi, 2 Agosti 2014
SERIKALI WILAYANI HAI MKOANI KILIMANJARO YAKEMEA VIKALI UNYWAJI POMBE WA KUPINDUKIA.
Serikali wilayani Hai imewaasa wananchi kuachana na tabia ya unywaji wa pombe uliokithiri
Serikali wilayani Hai imewaasa wananchi kuachana na tabia ya unywaji wa pombe uliokithiri ambao unaathiri nguvu kazi pamoja na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Novatus Makunga amesema kuwa wazazi pamoja na vijana wengi wanaokaa vijiweni wakiowemo madereva wa “bodaboda” ndio kundi linalosadikiwa kukithiri katika unywaji wa pombe aina ya gongo na viroba ambavyo vinatishia kuathiri mfumo wa uzazi.
Amesema kuwa pombe hizo ni kali, sio salama na hazina na nchi nzima inaweza kukosa nguvu kazi kutokana na vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kupungua au kutokuwa na nguvu ya kufanya kazi inavyopaswa kutokana na hali yao ya unywaji wa pombe hizo zisizo salama.
Katika kukabiliana na hali hiyo, Makunga amesema kuwa tayari wilaya yake ipo katika hatua za mwisho kukamilisha sheria sheria ndogo ndogo inayopiga marufuku unywaji wa pombe wakati wa saa za kazi wilayani humo.
MWISHO
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni