Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 2 Desemba 2014

WFP YASITISHA MSAADA WA CHAKULA KWA WAKIMBIZI NCHINI SYRIA.

WFP yasitisha msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Syria Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetangaza kusitisha msadaa wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi milioni moja na laki saba wa Syria walioko katika nchi jirani.WFP imesema wakimbizi hao wa Syria walioko Jordan,Lebanon,Uturuki na Misri huenda wakakabiliwa na njaa msimu huu wa baridi kali iwapo wafadhili hawatatoa kwa dharura kiasi cha dola milioni 64 zinazohitajika kununua chakula kitakachotumika mwezi huu wa Desemba. Kamishna wa umoja wa Mataifa anayeshughulikia maslahi ya wakimbizi Antonio Gueterres amesema wanatoa wito wa dharura kwa jumuiya ya kimataifa kuifadhili WFP ili wakimbizi wa Syria wasikabiliwe na njaa.Wengi wa wafadhili hawajaweza kutimiza ahadi walizotoa kuchangia katika kuwasaidia wakimbizi hao.Mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Finland na Sweden wamesema nchi zao zitajaliza pengo lililopo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni