![20141211_180103](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sTC_dPI96jdykaQPxONd1GBjYt75abCaZoyPFP4uOx4dOYpDCmrbdJoKWKNr7uFZnYGeT5xj749OBuBDBsZSwze4ObWcyEasnTeBee4h2zPttlHh5GUfyJNj2AYKRYf9l9t8t7qOjU1PzmY_Ks0XWZAuX8mOnhpTdyHnsOIk2f=s0-d)
Mjadala wa Wabunge wa Kenya uliofanyika jana jioni December 11 umeisha kwa mtafaruku baadha ya Wabunge kutoridhiana kuhusu kubadilika kwa baadhi ya vipengele vya Sheria ya Usalama ya nchi hiyo ili kupambana na matukio ya kigaidi ambao yameonekana kushamiri hivi karibuni.
Baadhi ya Wabunge waliounga mkono wanaamini kwamba mabadiliko hayo yatadhibiti vitendo vya kigaidi wakati wale wanaoipinga wanasema Sheria hiyo itaathiri Uhuru wa Wakenya.
Sheria hiyo imewasilishwa leo ndani ya Kikao cha Bunge na kuanza kujadiliwa.
Hali ya Usalama wa Kenya imekumbwa na changamoto mbalimbali baada ya kufululiza kwa matukio ya mashambulizi ya kigaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni