![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEguei9W2ky3-uCTp5DJoLQtp19aAyR2P-0ePbl_gqMnRffCV88y9wH09wxDVmTkXZb-v981qYnHIAGmAg71Q09gMlkQoZ3Y1aCk-aEwKHinHJfh8PtoEty2rR9ugdIVBBGh45vTWSmjb8II/s640/DSC_5027.JPG) |
KATIKA PICHA HUU NDIO UONGOZI WA TIMU NZIMA YA IDEAL HEALTHCARE SERVICE CENTER NA BAADHI YA WATUMISHI WAKE. |
Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika
kushiriki semina mbalimbali zinazotolewa na wakufuzi wa ujasiriamali ili
kuboresha kipato kitakachowasaidia kukuza uchumi na kuboresha maisha yao.
Hayo yamesemwa na mkufunzi
wa chuo cha elimu kwa wote kutoka katika kampuni ya IDEAL HEALTH CARE SERVISES Bw.Saravai Rashid kufuatia
mwendelezo wa semina ya siku nne inayoendelea mjini Moshi katika ukumbi
wa kanisa la WINNERS CHAPEL INTERNATIONAL na kuwakutanisha wadau mbalimbali wamaendeleo
na wajasiriamali katika sekta tofautitofauti.
Mkufunzi huyo amesema kupitia kampuni hiyo imelenga kuwainua
wananchi kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zinazowazunguka sambamba na
kuwajengea uwezo washiriki kuweza kujiajiri wenyewe na kuondokana na lindi la
umaskini linalochangiwa na dhana ya uwajibikaji hafifu wa rasilimali fedha na
uhaba wa maeneo ya uzalishaji.
Akifafanua zaidi amesema miongoni mwa mafunzo wanayowapatia
washiriki hao ni pamoja na elimu ya kilimo,biashara,mapishi na afya.
Akizungumzia swala la kilimo na ufugaji amesema washiriki
wanajifunza kitaalam kuendesha kilimo cha mlonge viazi vitamu vyenye vitamin A ,uyoga,ufugaji
wa kuku,sungura,samaki pamoja na utayarishaji wa vyakula vyake.
Akizungumzia kuhusu elimu ya biashara amesema ni pamoja na utengenenezaji
wa batiki ,makapeti sabuni aina zote,mafuta yenye virutubisho,utengenezaji wa
mishumaa ya kuuwa mbu sambamba na kujifunza
mbinu mpya zitakazowajengea uwezo washiriki kufanya biashara kwa tija na
kuziingiza bidhaaa hizo katika soko la Afrika
ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika soko la hisa na hatimaye kuweza
kusonga mbele zaidi katika kuanzisha viwanda vidogovidogo na kutatua changamoto
za ukosefu wa mitaji kupitia wafadhili na kupata mikopo katika taasisi za
fedha.
Kwa upande wa afya amesema ni pamoja na usindikaji wa
mbogamboga na matunda bila kuondoa virutubisho lishe,upishi wa keki,biskuti,mikate
na juisi kwa kutumia viazi lishe,usafi binafsi wa afya na ulaji bora.
Kwa niaba ya washiriki hao Bw.Yusuph Shimbi amesema wamefurahishwa na mafunzo hayo yanayoendelea
kwa uweledi wa juu zaidi kutoka kwa
wakufunzi mbalimbali kwa kuzingatia ubora wa uelewa kwa washiriki kwani yeye binafsi
amekua akijishughulisha na ufugaji wa sungura na amekua akipata hasara kwa kuwagharamia
mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula na tiba lakini kupitia mafunzo hayo waliyopatiwa
amekua na ufahamu wa kitaalamu utakaomwezesha kupata faida mara dufu.
Hata hivyo kwa upande wake mgeni rasmin katika ufunguzi wa
semina hiyo Mh.mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amewataka washiriki
kuzingatia yale yote waliojifunza katika mafunzo hayo sambamba na kuwaahidi kuwa
serikali ya awamu ya tano inaendelea kuzishughulikia na kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili wajasiriamali wadogo ikiwemo swala la ubora wa vifungashio
vinavyoshusha thamani ya bidhaa,upatikanaji wa mitaji na kuwataka wananchi
kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa na watanzania ili kukuza uchumi wa
viwanda vidogovidogo.
TAZAMA MTIRIRIKO MZIMA WA SEMINA HIYO BAINA YA WAKUFUNZI NA WASHIRIKI.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjYTfaSGVKx3Gt2yoXmAuknj3lkdZI2HYyFi0f1qbjzkREBRy1oU0De3GqACuMbJy0BNJvsoJ_TrkkqeNnpu0AL-nbYgF6dSn_y7eAyGo1jd6N4NMZxho_YzfbLqS6pHZEBu5fYSYxu-XxM/s640/DSC_5173+-+Copy.JPG) |
DR.JOHN KABUGI AKIFUNDISHA SOMO LA KILIMO. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhVDWqRFcfYsz6cgh2c0GEtegFs6KDWjFYWAfwP5cskkadxk4Ex-tPbCccxJH4zuiPl0hUdhRc-4ay76qQ6fx2AchAB2p7TsJpeHuNNYHfQk0G55XHEilE8dSZalfx3aqBpnJs6GTZIhkSl/s640/DSC_5032+-+Copy.JPG) |
ALIYESHIKA KIPAZA SAUTI NI MKURUGENZI WA IDEAL HEALTHCARE SERVICES CENTER AKIFANYA UTAMBULISHO WA TIMU NZIMA KULIA KWAKE NI MKUFUNZI WA KILIMO BW.MIKE PEENS,KUSHOTO KWAKE NI DR.ESTHER MTWALIZYA ,DR.SARAVAI RASHIDI NA WANAOFWATA NI BAADHI YA WATUMISHI HIYO (JOYCE KISANGA,LILY SAIMON NA MWISHO KABISA NI GLADY KISANGA.) |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEih360ndvARPZpHiSFjoOayljZSvRoW7cPcMKcTxriFWj0rDDeBWYBD2bEyU8BU9qFq0a0oVYtAPWNsVvDELlINzViKpPUBFoxxUQpTF2_wU9rmIwSJZKfwiAKaWwj2bTwGfrfkSbzgeepn/s320/DSC_5026+-+Copy.JPG) |
HUYU NI MKUFUNZI MCHUNGAJI EMMANUEL ELIAH AKIFUNDISHA SOMO LA UCHUMI. |
|
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgM0QK6ycKegEyEZXxLjEEnPo-74sbhZYBaUraT7IYIwD0x8wjUBtfeUDUcihVngvGJL8L9gb2FB9Aq4mom9WeOAlFxIeSJUZY2SabO1GRlnyW9hczISgNgNNTAe4d9nvFnsv7K5HVAMjbr/s640/DSC_5083+-+Copy.JPG) |
KATIKA PICHA NI MKUFUNZI DR.JOHN KABUGI AKIFUNDISHA SOMO LA UFUGAJI WA KUKU WAKIENYEJI KITAALAM.
|
|
|
|
|
|
|
UNAOWAONA NI BAADHI YA WASHIRIKI WAKIWA WANAMSIKILIZA DR.KABUGI.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBX9wwGyyX6BG1Inxr47MdqBMzEEnI2tz_kfG0mjnWfY57pjJAw0lIGBi7PqgTUv2ZfgZdT86o0rTVZxzvG6M6Ye8ee5p5yyLhg3-EgACnTIzlIDKgmEX38FV3cCTNa0Tvnnxmv3KJbwkY/s640/DSC_5167+-+Copy.JPG) |
DR.SAVARAI RASHID AKITEMA CHECHE JUU YA MWONGOZO WA KUPIKA ICE CREAM. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjyRArg-rSv5Wo83TxEmEqvYSYyFqd_hq1-QS2J7XdbkAMPQHh8qiJzSaplzY1wx_tw08FWFnrJy1kYThB2X0acQZ4qL1x5UGJPFS5a6H5XNvvOcqVzz-kSykD2gr7SfvcLjkPbbTD8VHEz/s640/DSC_5183+-+Copy.JPG) |
MKUFUNZI DR.RASHID AKIWAELEKEZA WASHIRIKI KWA VITENDO. |
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhre_pjRxb1RhT840tYcCLVqSE7is00DxpOQN4BFnlV-l_Vp4qyG1sNExvQD2oP_zDU9fULaB5o-29YXxK__zUZyzWelVzB7I5cdX1VXB0nUHPUcNfQNUln3FjHKCP5CsR2HtSfR8dCZrfl/s640/DSC_5194+-+Copy.JPG) |
UNAOWAONA KATIKA PICHA NI WASHIRIKI WAKIFANYA MAZOEZI KWA VITENDO. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEisu9KLusSsKDnsqeEBiHVAqurSgpA2I-VelWSjTQcoodtzyxTaa-GjyNHR00G-fbGt0Ch3kpJO1OAOeWz1bxAr7dVuiq5nl1AxS63X9bIbT2tDgRjH7TWhuM_iYPn1ULSdejFT4m3HDN5M/s640/DSC_5181+-+Copy.JPG) |
WASHIRIKI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA NA KUTAZAMA WANACHOKIFANYA BAADHI YA WENZAO. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiEmy1DIkZNNYBBpIN4UoUmU-P-VtwuU7du0OAx5Cm_gaKLZaPuPfixoODGp9eCCX_JF4Uz5c5fNsT9jNkJ99-OcmnchyuoxMzFnH5MDBTrOESuwFN_-Sg_Wh14Y6B8rgRbL_vlEKB8iZIq/s640/DSC_5208+-+Copy.JPG) |
UNAYEMWONA KATIKA PICHA NI MKUFUNZI AFISA BIASHARA MKOA WA KILIMANJARO BW.JAMES LISUNGU AKIFUNDISHA SOMO LA BIASHARA. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhx7oOrMNRvsqPNn2IIPaZuEi-jjwktQezYhbUAB-DQFPRb6RaddUPOFjW8DVQXJGnTcM3Q05vUrucLDRBxpIdiY84Hc7Sul5Ns53j0lG-2uFtdhai4IL8qn8pclSekjGRRw1a9Zw0Mg0T/s640/DSC_5216+-+Copy.JPG) |
WAFUATAO NI WASHIRIKI WA SEMINA HIYO WAKISIKILIZA MBINU MBALIMBALI ZA KUFANYA BIASHARA. |
HUYU NI MKUFUNZI DR.KABUGI AKIFUNDISHA SOMO LA KILIMO.
UNAYEMWONA KATIKA PICHA NI MSHIRIKI AKIULIZA JAMBO KUHUSU KILIMO.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjNps8KsKYBxkAH5ZwAbRJx1njYO_jRFLeEPxAr2zWHlVMfN3Sgm-oh6WT9kuPYoaQ7zjouYamrlxPzhI10dZPfSWZqMKX7Xg4127VEJgfRO3u5jwJ-a1X6TKJJAGvrgBdo8aTC3sJwHwyR/s640/DSC_5232.JPG) |
MKUFUNZI DR. RASHID AKIFUNDISHA SOMO LA BATIKI. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZZThjFZ53vYKZXR-UBEZlSbobugttHzdBAs0IQ0e55vElKE7nigVoq267cR9Psf3jMFHnek9k9kwJqwQJMi0qLSKdHZXAtNtEjUggxohovHcOacgy-XmNhV8Fz6C7ZMShGPDDvUqZVrr_/s640/DSC_5228.JPG) |
HAYA NI MAPOKEZI YA MH.MKUU WA MKOA WA KILIMANJORO ANNA MGWHIRA. |
|
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTRbZRHXRog-H1g_k5gYXTDPEld5rVzPTmnzqhcaWE27CGM9OEr3rA-cnA4Tox3a08WEbW9QiKCxYYZxaqcc7sM5Cit_9autMeoWDQiUWVFHnno35WW-91E484C3RXKIskhHdcfJkfNGFM/s640/DSC_5241.JPG) |
WASHIRIKI WAKIWA NA UTAYARI KUSIKILIZA HATUA ZA UTENGENEZAJI WA BATIKI. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPXAtpoWr9iBimrcrhRaHqYPKRy7HYk6hh7dU8RwnkkltDb6XjfEXEmcbf1bqIOCNcp_fRAoLglG3R5JaWZKnige1MDxpcIweRZRFx7mXKC_VlvhF-HZfthxIwRmXw_v3RurQlFOXwCMFV/s640/IMG_7394.JPG) |
MKUU WA MKOA ANNA MGHWIRA AKIFURAHIA MAUDHURIO YA WATU WALIOSHIRIKI. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj7eqswv-o-544NGKd1JBNIMHya8ua4A5YuPwz2LzpidnKAFsYO7hMg-U6C1c7ob2zW0cI3o1FRuh_5H2JViXTd90jeOcFZp5_hC5ui7VolEd6jz0zb3mhPyTx8EF6H-9yjh9uOQuXTM53k/s640/DSC_5251.JPG) |
MH.MGHWIRA AKIELEZEA JINSI ALIVYOKUA AKISHIRIKI HAPO AWALI KATIKA UJASIRIAMALI WA USUSI WA NYWELE. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhSyYCpTDDC2IpO4zGztv6YgioeXSw3aVJAB6YwLMdv0rkbCSzoGxnPV4E7xo3f_og-dLmTRnEn_V5yx_SlfUEQHCYgtRsGh-RXHEi_yRCWyei7pBPQAUeCp0rWBiI_MPHloai-TdkbBjPy/s640/IMG_7389.JPG) |
MH.MGHWIRA AKIWATAKA WAJASIRIAMALI KUTOKATA TAMAA KWANI NI WANUFAIKA WA KESHO. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhpAWcvA6t1r6WbWHaZl0tzwlMOIvsfjVKjunv3sMIqHilPz_gh9Y3qNOFspxDFmgeOARWJjW6jqa7qbIckVRATl-n-3wF4SmbOq1TPugobDw0BnFM_BrgFzGCojH1dKTDkNX04lfrZCG3/s640/IMG_7414.JPG) |
WASHIRIKI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA UJUMBE WA MKUU WA MKOA. |
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhQeeE71hwrgKOpTHZIOn7ewEsha0_6P6zRgdZvg4s0pj1r5Pg_khGh2q11CdbXdj1bj6c-hr05jbImLzE25S3MDPEpDo3BJUTrmq6RGDGnp19KHnLhhEKnGwhalZvRxRrm4tIFrGDjhHcm/s640/DSC_5210+-+Copy.JPG) |
MKUFUNZI DR.RASHID AKIWAELEKEZA WASHIRIKI JINSI YA KUNAKSHI BATIKI
.
KATIKA PICHA HAWA NI BAADHI YA WASHIRIKI WAKIMLAKI MH.MKUU WA MKOA.
DR.SARAVAI RASHID AKIWA ANAMKARIBISHA DR.KABUGI ILI KUMKARIBISHA MH.MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO KATIKATI HAPO NI DR.ESTER MTWALIZYA NA PEMBENI YAKE NI MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO ANNA MGHWIRA. ![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjS53sPomq3G-aSNQLCMRa0Pt6qbHYZuu8tyBk5CZpBWbbdfvPlH9KeR3WUM4fWm3up2swezVWXCZ0pFkIIRJsMwSXUkVeCAH1WSKbDD7qa19ZpT9tyWAr11LCK8Sb3jdiDMxWtOHojmmnC/s640/DSC_5249.JPG)
DR JOHN KABUGI AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA.
MH.MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AKIZUNGUMZA NA WASHIRIKI.
MH..MGHWIRA AKIELEZA MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUHUSIANA NA WALICHOJIFUNZA.
DR.KABUGI AKITILIA MSISITIZO MAMBO MUHIMU YALIYOZUNGUMZWA NA MKUU WA MKOA.
DR.KABUGI ,MKUU WA MKOA NA DR ESTER MTALITIZWA.
MKUFUNZI BI.SPERANCIA KAKUBA AKIMWELEZA MKUU WA MKOA JINSI YA CHIKO SANIFU LINALOTUMIA MIONZI YA JUA KUPIKIA VYAKULA MBALIMBALI.
TAZAMA JIKO HILO SANIFU LINALOONYESHWA NA MKUFUNZI HUYO .
TAZAMA PICHA ZA PAMOJA KATIKA GHAFLA HIYO.
PICHA YA PAMOJA YA MH.MKUU WA MKOA NA TIMU NZIMA YA CHUO CHA ELIMU KWA WOTE.(IDEAL HEALTHCARE SERVICE CENTER.
TIZAMA PICHA ZA WASHIRIKI WAKIPOKEA VYETI VYAO BAADA YA KUHITIMU MAFUNZO YA UJASIRIA MALI.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni