| Pichani aliyeshika kipaza sauti ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Dkt. Anna Mgwhira akisisitiza jambo katika ghafla za sherehe za Mei Mosi mwaka huu(2019). |
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mgwhira amezitaka Mamlaka
,taasisi na sekta mbalimbali kujitathimini katika kutoa huduma bora kwa
walengwa na kuziadhimisha sikukuu ya Wafanyakazi kama
chachu ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu kupitia huduma zilizotukuka .
Akizungumza katika
ghafla za sherehe ya Mei Mosi ziliyofanyika
kimkoa katika viwanja vya Chuo kikuu cha
Ushika mjini Moshi (MOCU)ameeleza kufurahishwa
na sherehe hiyo iliyovikutanisha vyama mbalimbali vya Wafanyakazi,Taasisi za
Umma ,Mashirika Umma na Wajasiriamali .
Mghwira amesema mbali
na kuwepo kwa fursa za ajira mkoani
Kilimanjaro Vyama vya ushirika vimekua
ndio chanzo cha kudhorota kwa sekta
mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo na biashara licha ya kuwepo kwa
changamoto kubwa iliyosababishwa na kufa kwa viwanda vilivyokua vikitoa ajira
kwa wananchi wengi .
“ushirika ndio umeua viwanda Kilimanjaro,Ushirika ndio umeua
Mashamba ya Umma Kilimanjaro,Ushirika ndio umesababisha kuyumba kiuchumi kwa
benki ya Ushirika na kupelekea kutofanya kazi kwa faida takribani miaka miwili
sasa licha ya kuwepo kwa wasomi Maprofesa
katika Ushirika , kazi ni ushuhuda ndugu
zangu”amesema mkuu huyo.
Akifafanua zaidi amesema kupitia hilo serikali imekua na
mikakati thabiti ya kuboresha miundombinu rafiki ya uwekezaji katika mkoa huo
kupitia sekta jumuishi na kupanua wigo wa ajira kwa wazawa sambamba na
kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinaadamu
ili kulinda rasilimali za taifa zinazopatikana ndani ya mkoa ikiwemo uwepo wa uoto
wa asili unaoitangaza nchi yetu katika
soko la utalii.
Katika hatua hiyo Dkt. Mgwhira amewatunuku vyeti na zawadi mbalimbali baadhi
ya wafanyakazi kupitia kada mbalimbali kama moja ya alama ya uwajibikaji na
utekelezaji wa majukumu yao wanapokua kazini.
Sherehe hizi za Mei mosi zinalenga kuwakumbuka baadhi ya wafanyakazi
duniani waliopata kadhia mbalimbali wakiwa katika majukumu ya kutekeleza wajibu wao
ambapo kauli mbiu kitaifa mwaka huu ni “TANZANIA YA UCHUMI WA KATI
INAWEZEKANA ,WAKATI WA MASLAHI BORA KWA WAFANYAKAZI NI SASA “
FUATILIA KWA UMAKINI MTIRIRIKO WA TUKIO ZIMA; HAYA NI MAANDAMANO YA WADAU.
| Pichani aliyevaa T.sheti nyekundu ni Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mhe.Agness Okororo na anayefuatia ni Mhe.Rosemary Senyamule mkuu wa Wilaya ya Same. |