![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmGHq0VFDRGF8B6sLYr85hxFo1z1C7CAL7D8duXbUSNvtPP833m1VX0BIaD5LmIiNzHXYsnLi-qPG3HhruiU_jpODXd6KL-lRGeaAbHFBdSUHHn8v_Mky1nCH49EkSNyr9vpy6xUDUP6oe/s640/bl.jpg)
HABARILEO
Utekelezaji wa shinikizo la kuvuliwa madaraka kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo linaloendelea kutolewa na Wabunge na kwa baadhi ya wanasiasa kwa Rais Jakaya Kikwete huenda ukaacha msononeko kwa wananchi walionufaika kwa kipindi kifupicha uongozi wa Waziri huyo.
Muhongo aliyejitengenezea uadui na wafanyabiashara na wanasiasa kutokana na misimamo yake ya kulinda maslahi ya umma na kuzungumzia ukweli huku akijiamini kulikotafsiriwa kuwa ni dharau hatma ya uongozi wake po mikononi mwa Rais ambaye ameshauriwa na Bunge kutengua uteuzi wake.
Baadhiya wananchi walisema Waziri huyo amefanya kazi kubwa na ya kimaendeleo kwa kipindi kifupi alichopewa majukumu na moja ikiwa ni kusambaza umeme katika vijiji vingi na kudhibiti ubadhirifu uliokuwepo hapo awali.
Pia amefanya juhudi kushawishi Watanzania ambao ni wataalam wa gesizaidi ya 10 wanaofanya kazi nje ya nchi hususani Canada na Uingereza mpaka wakakubali kurejea na kufanya kazi hizo nchini.
MZALENDO
Serikali imesemahadi sasa inakabiliwa na deni la bilioni140 lililosababishwa na uzembe pamoja na ubadhirifu katika Shirika la ndege la Tanzania ATC.
Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe alisema Serikali inakusudia kulipa deni hilo kwa mkupuo hadi litakapopungua zaidi ili kutoa nafasi ya kuimarisha upya sekta ya usafiri wa anga nchini.
Alisema imefikia wakati sasa Tanzania inapaswa kuwa na Shirika imara la ndege ili kuepuka kurudia uzembe na ubadhirifu uliojitokeza miakaya nyuma ATC.
Alisema Serikali itahakikisha Kila Mtanzania anatumia usafiri wa anga na si matajiri pekee kwa kuwa ipo kwenye mchakato wa kumalizia upanuzi wa viwanja vya ndege ilivyoanza,ikiwemo kujenga viwanja katika Mkoa ambayo hana kama Tanga,Shinyanga,Mara na Ruvuma.
MZALENDO
Serikali imesema kuwasili kwa mabehewa mapya ya treni 72 kutaiwezesha kampuni ya TRL kuimarisha safari za kusafirisha abiria kwenda Mikoa ya Mwanza na Kigoma mara tatu kwa wiki.
Pia kutokana na ubora wa mabehewa hayo,TRL inataraji kuanzisha treni maalum kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza na Kigoma itakayosimama kwenye vituo vikubwa pekee.
Mwakyembe alisema treni hiyo itakua na uwezo wa kusafiri kwa muda mfupi zaidi kulinganisha na safari za sasana alisema lengo la Serikali ni kuimarisha usafiri wa reli na kuifanyaTRL ijiendeshe pasipo kutegemee ruzuku kutoka Serikalini.
Aliongeza kuwa mabehewa hayo yalinunuliwa na Serikli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji mpango wa matokeo makubwa sasa,ambapo mabehewa 274 yamekwishanunuliwa na kugharimu zaidiya bilioni200.
MZALENDO
Mweka Hazina wa Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza anadaiwa kukiuka maadili ya uongozi na kujipatia masurufu na posho za kujikimu zaidi ya milioni nane kwa njia ya udanganyifu.
Habari kutoka ndani ya Manispaa hiyo zilizothibitishwa zinadai kuwa Lainie Kamendu alilipwa fedha hizo kwa awamu tano katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/14.
Alilipwa kwa ajili ya majukumu mbalimbali ikiwemo kwenda jjini Dar es salaam kufunga hesabu za Halmashauri yake kwa siku 50 ambalo aliliacha likiendelea na kurudi Mwanza kuchota fedha nyingine.
Kwamujibu wa chanzo cha habari inadaiwa kuwa mweka hazina huyo alipata milioni3.2 kati ya milioni19.2 zilizolipwa kutoka akaunti ya OC kama posho ya kujikimu kwa siku 40 ambapo kila siku alilipwa 80,000 kwa ajili ya kwenda kufunga hesabu.
MWANANCHI
Ripoti mpya ya kimataia kuhusu hali ya Utumwa Afrika duniani imeitaja Tanzania kuongoza Afrika Mashariki kwa kuwa na watu zaidi ya 350,000 wanaotumikishwa katika maeneo mbalimbali nchini kinyume na utaratibu.
Waziri wa Maendeleo,jinsia na Watoto Sophia Simba alisema ni kweli kuwa wafanyakazi wa ndani wanatumikishwa sana hapa nchini ukilinganisha na nchi nyingine.
Ripoti hiyo ijulikanayo kama ‘The Global Slavery Index 2014′ iliyotolewa nchini Australia inaonyesha kuwa Tanzania inashikilia nafasi ya 14 barani Afrika na kuwa ya 33 duniani.
Uganda ndiyo inayoshikilia nafasi ya pili kwa kuwa na watu 135,000 ikifatiwa na Rwanda 83,600,Burundi 72,300 huku Kenya ikiwa na watumwa 64,900.
MWANANCHI
Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila amesema Licha ya Chama cha Mapinduzi CCM kuwadharau Watanzania na kuamini kuwa hawana madhara kwa ustawi wake, kashfa yawizi wa fedha akaunti ya Tegeta Escrow itaking’oa Chama hicho madarakani.
Kauli hiyo imetolewa na Mbuge huyo wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kuchukua hatua kutokana na mapendekezo manane ya Bunge yaliyotolewa na Ripoti ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi wa fedha hizo.
Kafulila alisema licha ya wnanachi kukerwa na tabia ya wizi na ufisadi wa mali za umma,bado CCM imeendelea kuwadharau kwa vile wananchi hao kila mara wanaunga mkono chama hicho.
Alisema nchi ipo njiapanda na hali ni mbaya kwa vile licha ya uchumo kuporwa na watu wachache,Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua stahiki wahusika na kuwapeleka mahakamani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni