Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 7 Desemba 2014

Taarifa kutoka Ikulu kuhusu Rais Kikwete leo Desemba 07

Tulisikia kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji Marekani, Rais Kikwete alipewa masharti kadhaa na madaktari waliomfanyia upasuaji juu ya utaratibu wa kufanya katika kipindi cha miezi mitatu, ambapo moja ya masharti aliyopewa ni kutofanya kazi ngumu. Katika ukurasa wa Facebook wa gazeti la Mwananchi, wamepost picha na story inayosomeka hivi; “..MAZOEZI: Rais Jakaya Kikwete akifanya mazoezi katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, kutekeleza ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara tatu kwa siku ili kuimarisha afya yake, baada ya upasuaji mwezi uliopita nchini Marekani. Picha na Ikulu..“

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni