Tafuta katika Blogu Hii

Jumatano, 9 Novemba 2016

TRUMP RAIS MPYA WA MAREKANI LICHA YA KUFEDHEHESHWA KWA MUDA MREFU NA WAPINZANI -RAIS MAGUFULI AMPONGEZA.

Leo November 9, 2016 Marekani imeweka historia nyingine baada Donald Trump wa chama cha Republican kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais. Rais Magufuli ametoa pongezi zake kwa Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake Twitter “ Congratulation President-Elect and people of America for a democratic election,I assure and people of Tanzania for a continued friendship. — Dr John Magufuli (@MagufuliJP) November 9, 2016 Donald Trump achaguliwa kuwa Rais mpya wa Marekani Donald Trump amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Marekani baada ya kumshinda mpinzani wake, Hillary Clinton. Tayari Clinton amempigia simu na kukubali kushindwa. Donald ameshinda majimbo ya uchaguzi 276, huku Clinton akishinda 218. Kushindwa kwa Clinton kumekuwa pigo kubwa zaidi katika maisha yake ya kisiasa hasa kwakuwa wengi walimtabiria ushindi na kuwa rais wa kwanza mwanamke. Akihutubia baada ya kutangazwa mshindi, Trump amempongeza Clinton na kusema amefanya kazi kubwa na kwa muda mrefu na kwamba anastahili kulipwa fadhila. Amewaomba Wamarekani hata wale ambao hawakumpigia kura, kumuunga mkono kwenye safari yake ya kulijenga taifa hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni