Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 22 Februari 2019

MAJALIWA ASISITIZA ELIMU JUMUISHI HAPA NCHINI AMPA KONGOLE DKT.MENGI.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Shule ya Sekondari ya  ST. Pamachius Inclusive iliyopo katika kijiji cha  Kimashuku wilayani Hai, Februari 22, 2019. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na wa pili kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Isaac Amani, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira na wa pili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wakuu wa Wilaya hapa  nchini kushirikiana na wazazi katika kuhakikisha wanawafichua watoto wenye ulemavu kwa lengo la kuwapatia elimu.

Ametoa wito huo mkoani Kilimanjaro katika ziara yake mkoani humo hii leo wakati akizungumza katika uzinduzi wa shule jumuishi ya secondari St. Pamachius Inclusive iliyopo katika kata ya Mnadani kijiji cha Kimashuku wilayani Hai.

Amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu wa aina tofautitofauti  kwa kutenga bajeti zenye tija ikiwemo kuendeleza miundombinu wezeshi katika  Chuo cha ualimu Patandi ambapo  mradi huo umegharimu  zaidi ya shilingi billion 2 za kitanzania .

Akifafanua zaidi Majaliwa amezitaka taasisi mbalimbali za dini na watu binafsi kujikita zaidi katika kuchangia ujenzi wa miundo mbinu wezeshi ,huduma za afya na mahitaji muhimu yanayotegemewa na makundi mbalimbali yenye uhitaji katika taifa  ambapo amempongeza Dkt.Reginald Mengi kwa kuwa mzalendo wa kwanza kuchangia huduma mbalimbali.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Padre Patrick Asanterabi amesema shule hiyo ilianza ujenzi wake tangu mwaka 2015 na kuanza kutoa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha Kwanza January 5 mwaka huu ambayo hadi sasa inawanafunzi 74, 34 wasichana na 40 waluvana.

Katika hatua hiyo Asanterabi ameishukuru Serikali na wadau wa elimu kwa mchango wao wa hali na mali katika kuhakikisha shule hiyo inayojumuisha wanafunzi wenye ulemavu na wanafunziwa kawaida  na kufikia malengo yaliyokududiwa na Askofu mkuu jimbo la Arusha Isaac Amani.
                 TIZAMA PICHA MUHIMU HAPA KATIKA UZINDUZI  HUO.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu  Isaac Amani wakati alipowasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive iliyopo katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai kuzindua shule hiyo, Februari 22, 2019. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa. 

 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira katika uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive iliyoyopo katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai uliofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Februari 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana  na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP,  Dkt. Reginald Mengi wakati alipowasili  kwenye Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive iliyopo katika kijiji cha Kimashuku wilayani  Hai kuzindua shule hiyo, Februari 22, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari ya  ST. Pamachius Inclusive  iliyopo katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai kabla ya kuzindua Shule hiyo, Februari 22, 2019. Kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha,  Mhashamu Isaac Amani.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Shule ya Sekondari ya  ST. Pamachius Inclusive iliyopo katika kijiji cha  Kimashuku wilayani Hai, Februari 22, 2019. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na wa pili kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Isaac Amani, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira na wa pili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe, Mary wakikagua madawati   kwenye  moja ya madarasa ya Shule ya Seondari ya  ST.  Pamachius Inclusive iliyopo katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai, iliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Februari 22, 2019. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Isaac Amani na kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Joyce Ndalichako.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amekaa kwenye dawati wakati alipokagua madrasa ya Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive  iliyopo katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai baada ya kuizindua Shule hiyo, Februari 22, 2019.  Wengine kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Isaack Amani, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Nadlichako na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira.
 Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza  baada kuzindua   Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai, Februari 22, 2019.
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza  baada kuzindua   Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai, Februari 22, 2019.
Baadhi ya wanafunzi  weye uhitaji maalum katika  Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai, Februari 22, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  akishuhudua mwanafunzi Joseph Mtei ambaye hana mikono yote miwili akiandika kwa kutumia vidole vya miguu  baada kuzindua   Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai, Februari 22, 2019.
Moja ya Darasa katika Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza  baada kuzindua   Februari 22, 2019.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya ST. Pamachius Inclusive katika kijiji cha Kimashuku wilayani Hai,wakitoa salaam kwa mgeni rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Februari 22, 2019.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni