Waziri Mkuu waJamhuri ya Muungano wa Tanzania , Kassim Majaliwa akivisisitiza vyombo vya usala kuhusu ulinzi katika mpaka wa holili. |
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya dola kuimarisha ulinzi wa kutosha katika mpaka wa Holili na kizisisitiza Mamlaka zinazohusika kutimiza wajibu huo kufuata sheria,kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali.
Akizungumza katika ziara
yake ya kikazi katika kituo cha Forodha
Holili, wilayani Rombo Majaliwa amesema serikali inatambua umuhimu wa mipaka
iliyopo wilayani humo sambamba na
michango muhimu katika kuhakikisha fursa
muhimu za kijamii zinafikiwa na kuleta tija kwa wananchi.
Akifafanua zaidi
amewataka wananchi wanaofanya shughuli za kukuza uchumi hususani katika sekta
ya biashara ndani na nje ya mipaka ya
Tanzania na Nchi jirani kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali ili kuimarisha na kuendeleza hali ya amani na
utulivu .
” Katika kukuza uchumi
wa taifa Serikali ina kila sababu ya kusimamia na kulinda mipaka yake hapa
nchini sambamba na kuhakikisha wananchi
wanapata huduma stahiki kupitia sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi hivyo
nawataka watumishi wa umma kushirikiana na wananchi kuwafichua wale wote
wanaojihusisha na biashara za magendo zinazosababisha serikali kukosa mapato pamoja na kuthibiti mianya ya rushwa ”. Alisema
Majaliwa.
Katika hatua hiyo Majaliwa
amewataka wakuu wa Idara hapa nchini
kushirikiana na watendaji wa serikali kupokea na kutoa ushauri wa kitaalaam katika kutekeleza wajibu wao kwa
wakati na kuhakikisha changamoto mbalimbali za wananchi zinatatuliwa na kuibua
fursa zitakazochangia ongezeko la ajira kwa wazawa .
“Serikali ya awamu ya
tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuchukua hatua stahiki kwa mtumishi yeyote yule Mvivu,Mla rushwa
,Mwizi,Mbadhilifu na Mzembe hivyo simamieni vizuri vyanzo vya mapato na
rasilimali muhimu katika ustawi wa uchumi”Alisema Majaliwa.
Akizungumzia kuhusiana
na swala la Pombe haramu zaidi ya 48 zinazotengenezwa wilayani humo ameziagiza kamati ya ulinzi na usalama kufanya msako mkali
haraka iwezekanavyo katika kubaini mitambo yote inayotumika na wahusika kuchukuliwa
hatua kali za kisheria .
“Awamu ya tano haipo
tayari kuona wananchi wake wanadhohofika afya zao kutokana na matumizi mabaya
yanayotokana na unywaji wa pombe ,tumedhamiria kuwahudumia wananchi katika
sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya hivyo sina budi kusema vyombo vya dola
kamata ,weka ndani, chunguza na wapelekeni Mahakamani”Alisema…..
TIZAMA PICHA HIZI JINSI MAJALIWA ALIVYOKABIDHIWA ZAWADI HII.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni