![]() | |
| Viongozi na Wadau Wanachama mbalimbali wa KDF |
Msuya amebainisha hayo kufuatia Mkutano Mkuu wa Mwaka wa KDF uliyofanyika mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa Maendeleo.
Akizungumza mara baada ya ghafla hiyo, Msuya amewataka wanachama wa KDF kuungana kwa pamoja na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro kupitia sekta ya viwanda na kuendeleza zao la kahawa ambalo limeonekana kufifia kutokana na kuyumba kwa vyama vya ushirika na kufa kwa baadhi ya viwanda vilivyochochea fursa za ajira na ukuzaji wa uchumi kwa miaka iliyopita.
" Changamoto kubwa iliyoibuka baada ya kushuka kwa uzalishaji wa kahawa walioathirika zaidi walikuwa ni wakulima wadogo,KDF iliundwa mwaka 2004 lengo ikiwa ni kuwaunganisha wakazi wa Kilimanjaro, Tawala za Serikali za Mkoa, wafanyabiashara na taasisi za kidini katika harakati zilizokusudiwa kushughulikia changamoto zinazowakabili Wanilimanjaro na jinsi ya kukabiliana nazo."
Akifafanua zaidi amesema mchango mkubwa wa KDF ni kuchochea gurudumu la maendeleo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo kuhamasisha umuhimu wa maendeleo ya jamii kupitia huduma mtambuka kwa kushirikisha taasisi za Serikali na mashirikaya umma na watu binafsi.
Katika hatua hiyo Msuya ameng'atuka katika nafasi ya uongozi ya Uwenyekiti wa jukwaa hilo la ukuzaji wa maendeleo mkoani Kilimanjaro baada ya kutumikia wadhifa huo kwa takribani miaka 15.
Katika hatua hiyo amewashukuru viongozi wenzake wa KDF kwa ushirikiano waliompa wakati wote wa uongozi wake ambapo amewahimiza wanachama wa mkutano huo kumpa ushirikiano mwenyekiti mpya Mh.Balozi Ibrahim.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa KDF, Bwana Mahmoud Mringo, amesema uongozi mpya utazingatia kuimarisha ushirikiano kwa kuzingatia uhalisia wa tasnia mbalimbali kama moja wapo ya kipaumbele kitachonchangia ushindani na kuibua fursa mpya za ajira.
"Kilimanjaro zamani ilikuwa mstari wa mbele wakati wa kutoa elimu ambayo ilikuwa ya hali ya juu lakini kwa sasa inaonekana kuwa inarudi nyuma, uongozi mpya wa KDF tutazingatia njia muhimu za kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ili kuendana na teknolojia iliyopo na kuongeza ufanisi katika utendaji na usimamizi wa miradi mbalimbali"
"Lengo letu litakuwa katika kuimarisha viwanda vidogo, na kuhamasisha uanzishaji wa viwanda vipya na ikiwemo vile vya zamani ili kuleta ushindani wa biashara zitakazoleta tija kwa ustawi wa ajira kwa wazawa "
FUATILIA PICHA ZOTE HAPA.



































Hakuna maoni:
Chapisha Maoni