Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 10 Mei 2019

TAMASHA LA UHAMASISHAJI UNYWAJI WA MAZIWA KILIMANJARO LAFANA SHIRIKA LA SNV LAWAKUTANISHA WADAU.


Maziwa salama chakula na pesa “Kauli hii inachukua nafasi yake katika kukuza uchumi wa wafugaji na kuboresha afya za watumiaji wa maziwa salama licha ya waliowengi kulalamikia gharama za kumudu kununua bidhaa hiyo adimu .
Jambo hilo ni kama anasa kwa watanzania walio wengi na haoni umuhimu wake kwa upande wa afya mwilini,ukweli ni kwamba baadhi ya watu wanapuuzia na hawaoni umuhimu wa kunywa maziwa hata kama yanapatikana kwa urahisi katika maeneo wanayoishi.
Wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa maziwa yana kazi nyingi mwilini ikiwamo kuifanya ngozi kuwa nyororo, kuimarisha meno na mifupa kutokana na vitamin zilizopo.
Shirika  la maendeleo la uholanzi CNV wameamua kuungana na wadau wa maziwa kupitia sekta ya usindikaji  na unywaji wa maziwa salama kwa lengo la  kuhamasisha unywaji wa maziwa na kuwakutanisha wadau mbalimbali  kujifunza na kuona shughuli muhimu zinazofanywa na wengine katika sekta tofauti na kuunda umoja wa wadau wa maziwa sambamba na kuzindua  jukwaa la unywaji wa maziwa   mkoani kilimanjaro.
Shirika la Afya Duaniani (WHO), linapendekeza kila mtu anywe angalau lita 200 za maziwa kwa mwaka ingawa wastani kwa dunia ni lita 108.
Tamasha hilo limeandaliwa na wadau mbalimbali wa maziwa wakiwemo wafugaji,wasindikaji wa maziwa, vyama vya ushirika na serikali .
 Madhumuni ya tamasha hilo ni kuhamasisha unywaji wa maziwa ,kuwakutanisha wadau mbalimbali na kuwaleta pamoja kujifunza na kuona shughuli muhimu zinazofanywa na wengine wa maendeleo katika sekta tofauti na kujua hali halisi ilivyo sasa katika mazingira tofautitofauti sambamba na kuunda umoja wa wadau wa maziwa na kuzindua  jukwaa la maziwa   la mkoa wa kilimanjaro.
Akizungumzia umuhimu wa shirika hilo  la CNV meneja mradi Bw.Tom Ole Sikar amesema kazi kubwa ya shirika hilo ni kuwaleta wadau wa maziwa pamoja ,kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji hususani katika upande wa  masoko kwa wafugaji na kupunguza umasikini unaosababisha na ufugaji usio na tija kwa kuwajengea uwezo  kuwawaezesha kuwapatia elimu juu ya ufugaji bora   kwa kuzingatia lishe bora,maji na nishati.
Akifafanua zaidi amesema katika tafiti zilizofanyika katika wilaya ya siha na hai ambapo mradi huo ndipo ulianzia rasmi  kuna jumla ya takribani ngombe elfu 53 wa maziwa na karibu kaya laki140 zinajishughulisha na  uzalishaji wa maziwa ambapo uzalisha takribani lita laki mbili na nusu kwa siku.
Amesema katika wilaya hizo mbili kuna jumla ya vyama vya msingi vya maziwa 14 na vikundi 8 vya  ushirika vikiwa na jumla ya wanachama 1500 ambapo kwa umoja wa vyama hivyo kwa siku vinauwezo wa kukusanya lita takribani elfu 24 kwa siku .
Akizungumzia swala la masoko amesema kwa umoja wa vyama hivyo wamekua na uwezo wa kusindika maziwa salama kwa walaji na kusababisha swala zima la unywaji wa maziwa kuwa na ongezeko kubwa na kutoa hamasa kwa walaji.
Hata hivyo akizungumzia changamototo mbalimbali ni pamoja na mwitikio hafifu kwa wafugaji kutokana na elimu duni juu ya ufugaji bora ambapo awali wafugaji hao walikua wanazalisha lita 5 -8 kwa siku ambapo kwa sasa shirika la SNV wameweza kutatua kupitia tafiti za mbegu bora ,ubora wa malisho,nishati lishe na kuongeza idadi ya uzalishaji wa maziwa kufikia lita 8-12.
Amesema kupitia changamoto hizo shirika hilo limeweza kuwajengea uwezo wafugaji ,wajasiriamali na wadau wa maendeleo juu ya ubora wa thamani  wa soko la maziwa ambapo kupitia elimu hiyo  wameweza kuyakutanisha makundi mbalimbali katika jamii  na kuwapatia fursa za ajira kupia sekta ya ufugaji bora,malisho na  soko la maziwa.














Hakuna maoni:

Chapisha Maoni