MBUNGE WA MOSHI MJINI JAFARY MICHAEL AKIWAHUTUBIA WANANCHI WALIOKUSANYIKA KATIKA MKUTANO WA ADHARA KATIKA VIUNGA VYA KIBOROLONI.
Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafari Michael amesema ni
vyema jamii ikatambua mchango mkubwa unaotolewa na viongozi pasipo kuangalia
itikadi za vyama vya siasa na kukubali kukosolewa pindi wanapokosea ili kujenga
fursa ya usawa na kuharakisha shughuli za maendeleo.
Akizungumza katika mkutano wa adhara uliofanyika katika kata
ya Kiboroloni na kujumuisha viongozi mbalimbali wa umma Michael amekanusha
kumekuwepo na kauli za kisiasa zinazowapotosha wananchi katika shughuli za
kukuza uchumi ikiwemo katazo la biashara ya mitumba kuendelea katika soko la Kiboroloni na kuathiri soko kuu la mitumba
Memorial ni uwongo mtupu.
Hata hivyo amesema kauli
hizo zinalishusha hadhi soko hilo kwa kulitangaza kuwa limekufa hali inayochangia kudorora kwa uchumi kwa
wafanyabiashara wadogowadogo alimaarufu kama machinga na kuwapunguzia dhana ya
uwajibikaji na kuwakatisha tamaa baadhi yao kutafuta maslahi yao kwa manufaa ya
kukuza uchumi na kuboresha maisha yao hali inayopelekea kuzorota kwa shughuli
mbalimbali, ukiukwaji wa haki na kunyanyasika kwa baadhi ya wajasiriamali pasipo
tija.
Akifafanua zaidi Michael amesema dhamira kuu ya Chama cha Demokrasia
na Maendeleo(CHADEMA)katika jimbo la Moshi mjini ni kupanua wigo wa uchumi kwa
kushughulikia vikwazo mbalimbali vinavyochangia kukwamisha na kukuza uchumi
sambamba na kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kupitia sekta mbalimbali
ikiwemo upungufu wa ajira unaosababishwa na kufa kwa viwanda mbalimbali na
upungufu wa miundombinu thabiti
unaopelekea kuzorota kwa shughuli za maendeleo ya jamii.
Akizungumzia swala la miundombinu ni pamoja na kufa kwa
reli ya TAZARA iliyokua ikitumika kutoka Tanga,Moshi,Arusha mpaka Musoma ambapo
ameshafanya majadiliano na waziri mwenye dhamana pamoja na mkurugenzi mkuu wa
shirika la reli Tanzania kupitia bunge la bajeti na kamati ya miundombinu ambapo
yeye akiwa kama mjumbe wameafiki kushughulikia kuikarabati reli hiyo kwa
kutenga fedha itakavyowezekana na hatimaye reli hiyo kuanza kutumika kusafirisha
mizigo huku mchakato wa ujenzi wa kisasa ukiendelea hapo baadae.
Akivitaja baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na Magunia ,Madawa na Kibo Match ambapo amesema amekua
akijitahidi kwa kiasi kikubwa kujenga hoja mara kwa mara bungeni na kuishawishi
serikali kuu kuhusu umuhimu wa viwanda hivyo na faida mbalimbali zitakazopatikana na hatimaye waziri mwenye
dhamana ameahidi kushughulikia swala hilo mara moja na kuwataka wananchi wa
Moshi kujiandaa rasmini katika fursa za ajira kupitia sekta ya viwanda.
HAWA NI BAADHI YA WANANCHI WAKIMSIKILIZA MBUNGE WAO KWA SHAUKU KUBWA YA KUFAHAMU MAMBO MBALIMBALI .
PAKUA SAUTI VIDEO NA PICHA BAADA YA MUDA MFUPI KUHUSU MKUTANO HUO BILA KUKOSA .


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni