Tafuta katika Blogu Hii
Jumapili, 27 Agosti 2017
WATU WAWILI MBARONI KWA KUMTOROROSHA MTOTO WA MIAKA MITANO.
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumteka na kujaribu kumtorosha mtoto aitwaye Julius Rajabu mwenye umri wa miaka mitano .
Akiwataja majina watuhumiwa hao kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Hamis Issah amesema ni pamoja na kolle kimoni miaka 40 mkazi wa nchini Kenya na Benjamini Masumbuko mfanyabiashara mkazi wa Dar es salaam miaka 36.
Hamis amesema watuhumiwa hao walifika nyumbani kwa mtoto huyo kijiji cha Ubungo(Jipe) mpakani mwa wilaya ya Mwanga na Mombasa nchini Kenya ambapo waliwarubuni wazazi wa mtoto huyo wakidai kuomba msaada na hatimaye kumtorosha mtoto huyo kupitia usafiri wa mtumbwi.
Akifafanua zaidi amesema wazazi wa mtoto huyo walibaini mtoto wao hayupo karibu na mazingira jirani walilazimika kutoa taarifa za kumtafuta mtoto wao ambapo kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro na raia wema walifanikiwa kuwakama watuhumiwa hao mnamo tarehe 23/08/2017 majira ya saa 4:45 na kuwatia mbaroni kwa uchunguzi wa tuhuma hizo.
Aidha amewataka wananchi kuwa makini na kuendeleza ushirikiano na jeshi hilo katika kutoa taarifa wezeshi zitakazosaidia kuwabaini waalifu mbalimbali na hatimaye kutokomeza matukio ya kiualifu hasa mipakani mwa nchi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni