Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 29 Agosti 2017

DK.REGINALD MENGI APIGA VITA RUSHA AMUUNGA MKONO MH.RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JOHN POMBE MAGUFULI.

PEMBENI HAPO KATIKA PICHA NI MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO BI.ANNA MGHWIRA. Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi hapa nchini Mh.Dk.Reginald Mengi amewataka wafanyabiashara wa mkoa wa Kilimanjaro kutokua na hofu ya ushindani wa kibiashara sambamba na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dk. John Pombe Magufuli kwa jitihada mbalimbali anazozifanya ikiwemo kupiga vita mianya ya rushwa inayolikabili taifa kupitia sekta tofautitofauti. Akizungumza katika kongamano la wafanya biashara mkoani hapo lililofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuwashirikisha wataalam pamoja na watumishi wa umma kwa lengo la kuainisha changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali kupitia sekta ya viwanda,kilimo na miuundombinu katika kuyafikia malengo yao na kuharakisha shughuli za maendeleo ya jamii. Mengi amesema ilikuyafikia malengo yenye tija wafanyabiashara wanapaswa kufuata kanuni ,taratibu na sheria za nchi katika kutimiza majukumu yao ikiwemo kulipa kodi kwa wakati,kuepu bidhaa za magendo zinazotengezwa hapa nchini na zile zinazoingizwa kinyume na sheria badala yake watumie fursa hiyo kuyafichua maovu katika mamlaka husika ili kulinda na kukuza uchumi wa taifa utakaochangia ongezeko la ajira, haki na uwajibikaji wa wananchi. Kwa upande wake msemaji wa kiwanda cha sukari Moshi(TPC) Bw.Jafary Swai amesema miongoni mwa changamoto kubwa wanazokumbana nazo ni pamoja na ukosefu wa miundo mbinu ya kisasa,upatikanaji wa masoko ambapo bidhaa zinazotoka nje zinazikandamiza bidhaa za ndani,taratibu za uhamiaji kwa wawekezaji wanaotoka nje ya nchi ambapo zinadaiwa kuwa na gharama kubwa sambamba na viatilifu vinavyotoka nje ya nchi na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima na kuathiri ubora wa uzalishaji. Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara mipakani mkoani Kilimanjaro Bi.Joice Ndosi amesema mbali na kuwepo kwa jitihada mbalimbali wanazozifanya wajasiriamali wadogowadogo na wafanyabiashara katika kukuza uchumi swala la vifungashio limekua ni kikwazo kikubwa kwao licha ya kuwa shirika la viwanda vidogovidogo hapa nchini (SIDO)linafanya kazi kubwa kuwafundisha wajasiriamali namna ya kuboresha ubora wa bidhaa na kumwomba Mh.Mengi kufikisha kilio hicho serikalini na kuzidi kuwekeza zaidi mkoani hapo. Hata hivyo Mengi ameahidi kukabililiana na tatizo hilo na kuahidi kuunda tume itakayotatua changamoto hizo kwa wafanyabiashara sambamba na kuunda tawi imara la wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro na kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kupitia maeneo ya uwekezaji yaliyopo kisheria hususani katika viwanda vilivyokufa kikiwemo cha Twiga chemichals,Kilwood,Kibo Match na Kibo paper.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni