Akizungumza katika ziara ya kushitukiza katika wilaya ya
Rombo na Marangu Mghwira amesema njia pekee ya kujenga mahusiano na ujirani
mwema baina ya wananchi na shirika la uhifadhi KINAPA ni ushirikiswaji wa mambo
muhimu yanayotarajiwa kufanyika sambamba na kutoa taarifa kwa wakati juu ya
vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya wananchi kinyume na utaratibu wa
sheria.
Mgwhira amesema anatambua jitihada za hali na
mali zinazofanywa na wadau hao wa maendeleo kwa kuiunga mkono serikali katika kutambua umuhimu wa uhifadhi ambao ni pamoja na kuhakikisha mandhari na aina mbalimbali ya uoto wa asili unahifadhiwa ikiwemo uhifadhi wa wanyamapori kwa ajili ya Utalii, kuhifadhi wanyama wanaotishiwa kutoweka kama vile Sokwe, Tembo na Faru.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ubetu ambacho ni moja ya vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo wilayani Rombo wamesema kumekua na unyanyaswaji wa wanawake ndani ya hifadhi hiyo kila kuchwapo.
Akifafanua zaidi mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mama Silayo amesema baadhi ya wanawake wamekuwa wakichapwa kwa fimbo na askari wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro pindi wanapokutwa ndani ya hifadhi wakiokota kuni au kukata majani kwa ajili ya malisho ya mifugo..
Akijibu tuhuma hizo Kaimu Mkuu wa hifadhi hiyo Bw. Charles Ngendo amewahakikishia wananchi hao kuwa hifadhi hiyo ni salama kwa wale wote walioruhusiwa kuingia ndani ya msitu wa hifadhi na hawatopata madhara yoyote endapo watatimiza wajibu wao bila kukiuka sheria na taratibu za hifadhi.
Hata hivyo Ngendo amewataka wananchi waliofanyiwa vitendo hivyo wawasilishe malalamiko pamoja na ushahidi katika utaratibu rasmi ikiwa ni pamoja na kuonana na uongozi wa hifadhi mapema iwezekanavyo na uongozi hautasita kuwachukulia hatua watumishi waliotenda vitendo hivyo.
Aidha Ngendo amesisitiza viongozi wa vijiji vinavyozunguka msitu wa hifadhi watumie kamati za mazingira katika vijiji husika kuratibu namna ya kusimamia wanawake wanaoingia ndani ya hifadhi kutafuta mahitaji waingie kwa usalama bila ya kupata bughudha yoyote kwani maamuzi ya kulinda hifadhi yalipitishwa katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa (RCC) hivyo utaratibu huo hauwezi kukiukwa.
Hata hivyo wananchi hao waishio katika wilaya hizo wameishukuru serikali na hifadhi ya taifa KINAPA kwa kujenga mahusiano mazuri kupitia ujirani mwema ambapo wamekua wakinufaika na mambo mbalimbali yenye tija katika kukuza uchumi na ustawi wa maendeleo ya huduma za jamii .

Muikolojia wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) Imani Kikoti ( wa pili kushoto)
akimuelezea Mkuuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghwira mikakati ya hifadhi hiyo katika kuhakikisha uoto wa asili ndani ya hifadhi unalindwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira akiwahimiza
wananchi waishio katika kijiji Ubetu kuendelea kutunza hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro .
|
| Hawa ni Wananchi wa Kijiji cha Ubetu ambacho ni moja ya vijiji vinavyopakana na hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro wilayani Rombo. |
| TIZAMA PICHA ZA WANANCHI HAO. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni