MH.MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKIKATA UTEPE KATIKA UZINDUZI HUO. |
Makonda amesema kitendo hicho kinampa nguvu kama kiongozi wa mkoa huo kwa lengo la kukabiliana na matukio ya kiuhalifu katika kila kona za jijiji la Dar es Salaam.
Kiongozi huyo amesema magari hayo ni salamu tosha kwa vibaka,wahalifu na majambazi wote katika jiji hilo .
Makonda amesema uboreshaji huo wa magari ya Polisi utasaidia kuwahudumia wananchi wote wa Dar es salaam na kuhahikikisha amani na utulivu unaimarika katika kukuza uchumi ili kufikia malengo ya jiji hilo kufanya biashara ndani ya masaa 24.
“Magari haya sio ya kifahari muundo huu unalengo la kuboresha mazingira stahiki kwa askari wa jeshi la polisi kuona kila tukio linalotokea na katika mzunguko wa nyuzi 360 kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wote wa Dar es Salaam na kulinda uslama wao mara wanapopata matatizo ya kiusalama”alisema Makonda.
Akifafanua zaidi amesema lengo la kuongeza nguvu ya namna hiyo katika jeshi la polisi ni kuimarisha morali katika jeshi hilo na kwamba magari hayo ni kwaajili ya misako maalaum ya kuhakikisha wananchi wako salama na mali zao.
“Yatumieni magari haya kuwahudumia wananchi wa Dar es salaam kwa uwaminifu , ili pasiwepo mwananchi yeyote anapohitaji huduma msiseme hakuna gari,magari haya yalikua yamekufa kabisa kupitia ubunifu niliokuwa nao katika kumuunga mkono Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kubana matumizi na kufikia dhamira ya serikali ya viwanda kuelekea uchumi wa kati yaani Hapa kazi tu,niliwatafuta ndugu zetu RSA tukafanya majadiliano tukaanza kazi leo hii mnayaona magari haya yaliyokuwa yamekufa nimeyafufua na yanaonekana mapya.”amesema makonda.
Makonda amesema changamoto kubwa iliyokua ndani ya jeshi la polisini usafiri hali ambayo ilimfanya atumie jitihada kubwa katika kutafuta
njia mbadala ya kuhakikisha miundo mbinu inapatikana na Dar es salam inakuwa swari wakati wote.
Katika hatua hiyo Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kanda maalum ya Dar es salaam, (SACP)Awadhi Haji amempongeza mkuu wa mkoa huyo kwa ubunifu wa kipekee wakuliwezesha jeshi la polisi kanda maalamu kwa kupata ufumbuzi wa matatizo kadha wa kadha kupitia wadau mbalimbali.
Amesema magari hayo yalivyoletwa mkoani Kilimanjaro yalikua mabovu na yalikua hayawezi kutumika kabisa lakini leo yamekabidhiwa yakiwa mazima kutokana na kuboreshwa na kampuni ya RSA mkoani Kilimanjaro.
“Makonda amekua ni msaada sana kwetu alianza kwenye pikipiki na leo hii tunaona katika kuyafufua magari haya kwa kupitia kampuni ya RSA ambapo yatatumika katika shughui za kiusalama”amesema Haji.
Kwa upande wake mkuu wa mkao wa kilimanjaro,Anna Mghwira amempongeza RC Makonda kwa jitihada zake za kuhakikisha jeshi la polisi mkoani humo linakua na miundo mbinu ya kutosha.
“Nampongeza Rc Makonda kwa kukabiliana na vitendo vya kialifu sambamba na kugundua changamoto hiyo ya miundo mbinu mibovu ni kikwazo katika kuyafikia malengo ikiwemo vita ya dawa za kulevya hivyo kupitia tukio hilo ninaamini tutakuza uchumi wa watanzania kwa kutengeneza fursa za ajira na kusisitiza umuhimu wa hati miliki kama sehemu ya kulinda rasilimali za Tanzania”amesema Mghwira.
Kwa upande wake Meneja Masoko kampuni ya RSA ambao ndio watengenezaji wa magari hayo ya Jeshi la polisi mkoani Kilamanjaro,Melissa Foley alisema nafasi hiyo waliyoipata kuyafufua magari hayo ni moja kati ya mchango wao na kuiunga mkono serikali hapa nchini sambamba na kuwatambulisha zaidi kuwa wanaweza.
Amesema kuwa hii ni mara yao ya kwanza katika utengenezaji wa magari hayo ya Jeshi la polisi kupitia kampuni hiyo ambapo wameweza kuboresha magari hayo kwa muundo wa kisasa zaidi kwa kushirikiana na mkuu wa mkoa wa Dar es salam ambapo magari haya 14 ni katika awamu ya kwanza hivyo wanatarajia kutengeza magari mengine42 ya jeshi hilo la polisi katika awamu tofautitofauti.
TAZAMA PIZA ZA TUKIO ZIMA .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni