Tafuta katika Blogu Hii

Ijumaa, 20 Oktoba 2017

JESHI LA POLISI MKOANI KILIMANJARO LAENDELEZA KUTOA ELIMU KWA WADAU JUU YA SHERIA NA KANUNI ZA USALAMABARABARANI.


 Miongoni mwa shughuli muhimu katika kutekeleza majukumu yao jeshi la polisi ni kuwalinda raia na mali  zao,kusimamia amani kwa misingi iliyotuka sambamba na kujenga mahusiano mazuri juu ya upokeaji na utoaji wa taarifa na utoaji wa taarifa hizo sehemu husika.
 Kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyoadhimishwa kitaifa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro jeshi hilo limeendeza kasi zaidi na uweledi katika kuyafikia makundi mbalimbali kwa kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wenye dhamana kubwa ya kuwahudumia wananchi wakiwemo watumishi wa umma ,wananchi,makundi ya kijamii na kadhalika.
UNAYEMWONA HAPO MBELE AKIWA AMESHIKA KIBAO CHA ALAMA ZA BARABARANI  NI AFANDE (ASP)MOSSI NDOZERO MKUU WA KITENGO CHA ELIMU KWA UMMA USALAMA BARABARANI TANZANIA AKIWAELEKEZA WADAU MATUMIZI SAHIHI.
ELIMU HIYO INAHUSISHA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KAMA IFUATAVYO.

BAADHI YA VYOMBO VYA MOTO WAKIONYESHA USHIRIKI WAO.
BAADHI YA BODABODA MJINI MOSHI WAKIUNGA MKONO JITIHADA HIZO ZA JESHI LA POLISI.
KUPITIA JITIHADA HIZO MUHUIMU JUMLA YA WALIMU 200 KATIKA SHULE MBALIMBALI MKOANI KILIMANJARO WAMEPATIWA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI NA MKUFUNZI MKUU WA MAFUNZO HAYO MKOANI HAPA SAGENTI HILDA MLAY HUKU MAELFU YA WANAFUNZI WAKIWA WANUFAIKA.




 WANAFUNZI WANUFAIKA NAO HAWAKUA MBALI KUONYESHA UWEZO JUU YA UWELEWA WAO.





KATIKA HATUA HIYO MGENI RASM KATIKA GHAFLA HIYO YA KUONYESHA UWELEWA HUO KATIBU TAWALA MSAIDIZI UPANDE WA UTAWALA RASILIMALI WATU BW.SEBASTIAN MASANJA AKIMUWAKILISHA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO MH.ANNA MGWHIRA AMELAZIMIKA KUEZA KUWA AMEFURAHISHWA NA UELEWA WA WANAFUNZI HAO KATIKA ELIMU YA USALAMA BARABARANI.
KULIA NI BW.SEBASTIAN MASANJA KATIKATI KATIKA PICHA NI AFANDE (ASP) ALLY MOHAMED NA MWISHO HAPO NI AFANDE (ASP)MOSSI NDOZERO.
TIZAMA PICHA ZA PAMOJA ZIKIWAJUMUISHA WADAU NA VIONGOZI  HAO.







Hakuna maoni:

Chapisha Maoni