Serikali mkoani Kilimanjaro imetekeleza amri ya mahakama kuhalalisha kuuzwa kwa mnada ng’ombe zaidi ya 1000 zilizoingizwa kinyemela kutoka nchi jirani ya Kenya na kukamatwa katika kata ya Kiria wilayani Mwanga.
Mnada huo umefanyika katika soko la Mgagao wilayani humo kwa
kufuata kanuni ,sheria na utaratibu wa serikali hali iliyosababisha wanunuzi na
wananchi kusifia mwenendo mzima wa zoezi hilo.
Akizungumzia hali hiyo katibu mkuu wizara ya uvuvi na mifugo
Maria Mashingo amesema hatua hiyo ya
serikali itakua endelevu kwani kitendo hicho ni kosa la uhujumu wa uchumi na kufikia maamuzi hayo
itakuwa ni fundisho tosha kwa baadhi ya raia wakigeni kutumia vibaya mianya
iliyopo mipakani na kufanya uhalifu ikiwemo kuvamia maeneo ya nchi na kuendesha
shughuli za uchumi kinyume na sheria.
Mashingo ametoa wito kwa wananchi kuwa wazalendo kwa kuripoti
katika vyombo vyadola pindi wanapoona au kuwashuku raia wakigeni wasiowaaminifu
wanapoingia kinyemela ndani ya nchi na kuhodhi baadhi ya maeneo sambamba na
kuendeleza shughuli mbalimbali za kibinadamu na kuathiri uchumi wa wazawa hali
itakayosababisha uvunjifu wa amani na magonjwa ya milipuko.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira
amesema zoezi hilo limemalizika salama ambapo walilazimika kuwauza ng’ombe hao
kwa mafungu ya idadi ya ng’ombe 20 ili kuleta ushindani zaidi na kufanikisha
zoezi hilo mapema hali iliyosababisha amani na utulivu na jumla ya ng'ombe 1,065 waliuzwa kati ya ng'ombe1,115 kutokana na wengine kufa kwa kukosa huduma stahiki
.
Akifafanua zaidi Mghwira amesema jumla ya shilingi millioni 238,145,000 zilipatikana kutokana na mnada huo ambapo asilimia 7 alilipwa mdhabuni(dalali) wa mnada huo kwa mujibu wa sheria ya serikali hivyo ambayo ni sawa na shilingi 16,171,715 milioni , Halmashauri ya wilaya ya Mwanga walilipa 5,325,000 millioni kama ushuru hivyo serikali imebakiwa na shilingi 216,648,285milioni.
“kwa hiyo pamoja na kutoa gharama zote fedha ya serikali tuliyobakiwa nayo ni shilingi
216,648,285 ,million”alisema Mghwira.
Akifafanua zaidi Mghwira amesema jumla ya shilingi millioni 238,145,000 zilipatikana kutokana na mnada huo ambapo asilimia 7 alilipwa mdhabuni(dalali) wa mnada huo kwa mujibu wa sheria ya serikali hivyo ambayo ni sawa na shilingi 16,171,715 milioni , Halmashauri ya wilaya ya Mwanga walilipa 5,325,000 millioni kama ushuru hivyo serikali imebakiwa na shilingi 216,648,285milioni.
“kwa hiyo pamoja na kutoa gharama zote fedha ya serikali tuliyobakiwa nayo ni shilingi
216,648,285 ,million”alisema Mghwira.
Hata hivyo kwa baadhi ya wananchi walioshiriki katika mnada
huo wameipongeza serikali ya Tanzania kwa maamuzi hayo kama njia ya kutatua
migogoro iliyopo hapa nchini baina ya wafugaji na wakulima ambapo kutokana na
takwimu mbalimbali zinaonyesha kila kuchwapo kuongezeka kwa migogoro kutokana
na uhaba wa malisho na maji ambayo haikidhi mahitaji ya wazawa.
TIZAMA MWENDELEZO WA ZOEZI HILO KUPITIA PICHA ZIFUATAZO.
TIZAMA MWENDELEZO WA ZOEZI HILO KUPITIA PICHA ZIFUATAZO.
ALIYESHIKA KIPAZA SAUTI NI MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AKIFANYA UTAMBULISHO WA ZOEZI HILO.KULIA ALIYEVAA KOFIA NI MKUU WA WILAYA YA MWANGA BW.AARON MBOGHO. |
UNAOWAONA KATIKA PICHA NI WADAU WALIOFIKA KATIKA MNADA HUO KWA LENGO LA KUWANUA NG'OMBE HAO.
UNAOWAONA NI ASKARI WA JESHI LA POLISI WAKISIMAMIA ZOEZI LA KUTENGA MIFUGO HIYO KWA MAFUNGU YA NG'OMBE 20 KILA KUNDI MOJA.
HAWA NI WANUNUZI WAKISIMAMIA MIFUGO WALIYONUNUA SAMBAMBA NA KUKAMILISHA TARATIBU ZA MALIPO NA VIBALI VYA USAFIRISHAJI.
ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI KILIMANJARO WAKISIMAMIA AMANI NA UTULIVU KWA RAIA NA MALI ZAO .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni