Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 22 Oktoba 2017

MAADHIMISHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA KITAIFA MKOANI KILIMANJARO YAFANA SHERIA ZA USALAMA BABARANI ZASISTIZWA NA KUTILWA MKAZO.


Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika kitaifa mjini moshi mkoani Kilimanjaro yamemalizika salama huku wadau mbalimbali wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu wakionyesha kufurahishwa na utendaji kazi wa jeshi la polisi katika kutoa mchango wao katika kuzuia ajali za barabarani na kufanikiwa kupunguza idadi kubwa za ajali zinazotokana na uzembe wa madereva wasiowaaminifu ,ulevi uliokithiri na matumizi mabaya ya alama za barabarani.
Maadhimisho hayo yamemalizika katika uwanja wa Mashujaa na kuhusisha wananchi, wadau mbalimbali na viongozi wa umma.
Maadhimisho hayo yamemalizika kwa hari kubwa na uelewa kwa makundi ya kijamii sambamba na kukabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali kwa washriki walioshinda michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu na matumizi sahihi ya fasihi andishi kupitia shule za msingi.
 Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira ambapo alianza kwa kukagua mabanda ya maonyesho katika sekta mbalimbali na kupata maelekezo juu ya jitihada muhimu wanazozitumia wadau wao katika kuhakikisha wanapunguza ajali za barabarani zinasababishwa na hitilafu mbalimbali na ukiukwaji wa sheria za alama za barabarani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni