Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Anna Mgwhira amepiga marufu matumizi ya mifuko ya plastiki katika mkoa huo ikiwa ni njia sahihi ya kutunza na kuhifadhi mazingira.
Dkt.Mgwhira amebainisha hayo katika ghafla ya maadhimisho ya juma la elimu mkoani humo yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa dini,serikali na wadau wa elimu na makundi ya watu wenye ulemavu.
Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira katika kukabiliana na hali ya tabia ya nchi sambamba na kuwataka wananchi kutambua madhara makubwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira kutokana masalia ya plastiki.
Akifafanua zaidi amesema katika kukabiliana na katazo la mifuko ya plastiki wadau wanapaswa kuchukua hatua stahiki katika kuhakikisha Kilimanjaro inakua salama kwa kuonyesha ushiki wao kupitia huduma muhimu zinazopatikana katika ngazi ya vijiji,kata,tarafa,wilaya na hatimaye mkoa.
Katika hatua hiyo Mgwhira amevitaka vyombo vya dola kuunga mkono kwa kuwakamata watakao kaidi agizo hilo na kuchukuliwa sheria kama wahalifu wa makosa mengine na kuwafikisha katika mikono ya sheria.
Kwa upande wake Mratibu wa masoko kutoka kampuni ya Harsho Bi.Caroline Satsif amesema kampuni hiyo imeunga mkono agizo la serikali katika kukabiliana na athari mbalimbali zinazotokana na uchafuzi wa mazingira kupitia mifuko ya plastiki hivyo wamejikita katika kuzalisha mifuko rafiki wa mazingira kwa tija na kukidhi soko la walaji.
“Sisi kama wadau wa mazingira kutoka kampuni ya Harsho tumejikita kuzalisha mifuko rafiki wa mazingira ambayo kimsingi tunaamini mifuko hii itasaidia sana wananchi kukidhi mahitaji mbalimbali ya kubebea bidhaa mbalimbali kwa kuzingatia ubora wa soko la walaji hapa nchini mifuko hii ni ya bei nafuu na mtumiaji anaweza akatumia na baada ya hapo kama utakua umechafuka anaweza kuufua hata zaidi ya mara tatu kwa matumizi yajayo na baada ya hapo mfuko huu unaoza kabisa mithili ya karatasi , kwa sasa tunazalisha mifuko zaidi laki tano kwa siku hivyo tunaamini kutokana na katazo hili wananchi wa mkoa wetu na jirani hawatapata adha ya kushindwa kukudhi mahitaji yao kwa asilimia 100.”alisema Caroline Satsif.
Hata hivyo wananchi na wadau wa mazingira wamesema kupitia katazo hilo la mifuko ya plastiki hawana budi kuwaunga mkono wazalishaji hao wa mifuko rafiki wa mazingira kwani wanaamini muonekano wa mifuko hiyo itawavutia wengi kujikita katika matumizi sahihi na kuondokana na uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa .
TIZAMA PICHA KATIKA ZA WADAU WA ELIMU KATIKA GHAFLA HIYO.
Serikali ya Viwanda inawezekana Elimu na Ufanisi kwa Vitendo kwa matokeo bora. |
Katika picha ni Wafanyakazi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Maji na Maji Taka Moshi (MUWSA)Kushoto ni Bi.Sophia Kalist anayefuata ni Rashid Nachan anayefuatia ni Bi.Regina Mwanzoho. |
TIZAMA PICHA ZA BAADHI YA WADAU WALIOKABIDHIWA VYETI ,NGAO NA MEDALI.