Waziri wa Viwanda na Biashara,Joseph Kakunda amesema serikali haitaweza kuwavumilia wale wote walioshiriki kukihujumu kiwanda cha kukoboa kahawa kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro (TCCCo) sambamba na kuwachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kauli hiyo ameitoa baada ya ziara yake fupi ya kikazi alipotembelea kiwanda hicho , huku aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda hicho Maynard Swai na Meneja wake Mkuu, Adrew Kleruu wakiwa tayari wameshafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi.
Kakunda amesema Serikali ya awamu ya tano sio ya mchezomchezo na yeye kama waziri mwenye dhamana, hataweza kuvumilia wale wote wenye nia mbaya ya kuipaka serikali matope hivyo ,wote waliohusika kukihujumu kiwanda hicho na kuuza mali ya ushirika na kununua mitambao ambayo haifanyi kazi sheria itachukua mkondo wake na serikali itahakikisha mali za kiwanda hicho zinarudishwa zote ikiwemo nyumba moja na magari mawili ambayo bado hayajarudishwa.
“Wote waliohusika kukihujumu kiwanda hiki na kuuza mali ya ushirika na kununua mitambao ambayo haifanyi kazi sheria itende haki na sisi serikali tutahakikisha mali za kiwanda hiki zinarudi zote ,kuna nyumba moja haijarudishwa na magari mawili vyote hivi virudishwe na kuleta tija katika sekta ya viwanda na biashara kwa kutengeza fursa za ajira,”amesema Kakunda.
“Hiki kiwanda kilikua ni moja kati ya viwanda mama ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vinavyokoboa kahawa hapa Nchini,Tume ya ushirika ikiangalie kwa macho mawili kiwanda hiki kirudi katika heshima yake, tukienzi kiwanda hiki kama kiwanda kikubwa kuliko vyote Tanzania”amesema Waziri Kakunda
Akifafanua zaidi amesema ,imefika wakati Tume ya ushirika ikiangalie kwa macho mawili kiwanda hicho ili kiweze kurudi katika hadhi yake ya awali na kuwa rasilimali muhimu itakayokuza uchumi na kutangaza ushirika katika soko la ubora wa bidhaa sambamba na kuutaka Uongozi uliopo madarakani kwa sasa utoe fursa za ajira za kudumu punde kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji rasmi kwa wakinamama zaidi aliowakuta kiwandani hapo wakifanya kazi ya kuchambua kahawa .
“Ni matarajio yetu makubwa kuwa mfumo wa sheria utatenda haki,kwa walioshiriki kukihujumu kiwanda hiki kwani wamewahujumu wakulima kwa kiasi kikubwa ,leo hii nimeshuhudia mitambo ya miaka 60 katika kiwanda hiki bado inaendelea kufanya kazi vizuri janjajanja zilizokuwa zikitumika zilikua hazina tija sasa basi serikali tupo macho na tutapambana katika kuhakikisha kiwanda hiki kinarudi katika hali yake na ,”amesema
Hata hivyo Mwenyekiti wa kiwanda hicho,John Bhoshe amesema kiwanda kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiutendaji, ikiwemo manunuzi na matumizi mabaya ya Rasilimali za kiwanda hicho zilizotokana na uongozi uliopita hivyo kukisababishia kiwanda hicho hasara kubwa.
“Kati ya mwaka 2012 na 2014 yalifanyika mauzo ya nyumba 3 za kiwanda hicho,na magari 3 vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh.2.2bilion ambazo hazikutumiwa kwa shughuli za kiwanda inavyopasa ,matumizi ya fedha hizo yalikua mabaya na kudumaza maendeleo ya kiwanda hiki hadi leo,”amesema Bhoshe.
Akieleza hali halisi ya kiwanda hicho amesema kimekosa uwezo wa kifedha wa kujiendesha ambapo kwa sasa hali hiyo imeathiri shughuli za kiwanda hicho ikiwemo kushindwa kulipa madeni ya watoa huduma mbalimbali hivyo kupelekea madeni hayo kufikia zaidi ya sh1.2bilioni
Aidha amesema kuwa,Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1970 na Mjerumani na kilikua na uwezo wa kukoboa kahawa tani 50,000 kwa mwaka ambapo kwa sasa kimeendelea kushuka hadi tani 1,000 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vyama vya msingi vya ushirika kushindwa kukoboa kahawa kiwandani hapo.
Waziri wa Viwanda na Biashara,Joseph Kakunda amesema serikali itahakikisha wale wote walioshiriki kukihujumu kiwanda cha kukoboa kahawa Moshi(TCCCo) wanachukuliwa hatua kali za kisheria.
Wakati waziri akitoa kauli hiyo alipotembelea kiwanda hicho ,aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya kiwanda hicho Maynard Swai na Meneja wake Mkuu,Adrew Kleruu wamefunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi.
Aidha alisema kuwa ,wote waliohusika kukihujumu kiwanda hicho na kuuza mali ya ushirika na kununua mitambao ambayo haifanyi kazi sheria itachukua mkondo wake na kwamba serikali itahakikisha mali za kiwanda hicho zinarudi zote ikiwemo nyumba moja na magari mawili ambayo hayajarudishwa.
“Wote waliohusika kukihujumu kiwanda hiki na kuuza mali ya ushirika na kununua mitambao ambayo haifanyi kazi sheria itende haki na sisi serikali tutahakikisha mali za kiwanda hiki zinarudi zote ,kuna nyumba moja haijarudishwa na magari mawili vyote hivi virudishwe,”alisema Kakunda.
“Hiki kiwanda ni kiwanda kikubwa na cha mfano na kikubwa kuliko viwanda vyote vinavyokoboa kahawa hapa Nchini,Tume ya ushirika ikiangalie kwa macho mawili kiwanda hiki kirudi katika heshima yake, tukienzi kiwanda hiki kama kiwanda kikubwa kuliko vyote Tanzania”alisema Waziri Kakunda
Aliongeza kuwa ,Tume ya ushirika iangalie kwa macho mawili na kwa uangalifu mkubwa wa kiwanda hicho ili kiweze kurudi katika hadhi yake ya awali na kama mali muhimu sana ambayo iko chini ya ushirika.
“Ni matarajio yetu makubwa mfumo wetu wa sheria utatenda haki,kuhujumu kiwanda ni kuwahujumu wakulima,leo hii nimeshuhudia mitambo ya miaka 60 katika kiwanda hiki bado inaendelea kufanya kazi vizuri,”alisema
Naye Mwenyekiti wa kiwanda hicho,John Bhoshe alisema kuwa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maamuzi na matumizi mabaya ya Rasilimali za kiwanda zinazotokana na uongozi uliopita na kukisababishia kiwanda hicho hasara kubwa.
“Kati ya mwaka 2012 na 2014 yalifanyika mauzo ya nyumba 3 za kiwanda hicho,na magari 3 vyote vyenye thamani ya zaidi ya sh.2.2bilion ambazo hazikutumiwa kwa shughuli za kiwanda inavyopasa ,matumizi ya fedha hizo yalikua mabaya na yalidumaza maendeleo ya kiwanda hadi leo,”alisema Bhoshe.
Alieleza kuwa, kiwanda hicho kimekosa uwezo wa kifedha wa kujiendesha kwa sasa na kwamba hali hiyo imeathiri shughuli za kiwanda hasa kushindwa kulipa madeni ya watoa huduma mbalimbali na kwamba kiwanda hicho kina madeni ya jumla ya zaidi ya sh1.2bilioni
Kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1970 na Mjerumani huku kikiwa na uwezo wa kukoboa kahawa tani 50,000 kwa mwaka ambapo kwa sasa kimeendelea kushuka hadi kufikia chini ya tani 1,000 kwa mwaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vyama vya msingi vya ushirika kusitisha zoezi la kukoboa kahawa yao kiwandani hapo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni