Tafuta katika Blogu Hii

Jumanne, 28 Mei 2019

WAZIRI KAKUNDA KUWASAKA WANAOGHUSHI NEMBO YA RAJINDER (RSA )ATOA AGIZO KWA FCC.

Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh.Joseph Kakunda  katikati ni Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Bi.Aisha Amour Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Manmohan Bhamva.
Serikali hapa nchini imeigiza Tume ya ushindani hapa nchini FCC kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu wanaoghushi nembo ya kiwanda cha kuunganisha magari cha Rajinder (RSA)kilichopo Wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda katika ziara yake ya siku mbili mkoani hapa alipotembelea kiwanda hicho na kupokea changamoto zinazokikabili ikiwemo baadhi ya watu kughushi nembo hiyo.
“Kuanzia sasa nawataka muandikie barua rasmi ya malalamiko kwa Tume ya ushindani hapa nchini FCC haiwezekani watu wakatumia hati miliki ya mtu mwingine kinyume na utaratibu kujipatia kipato ,hivyo naiagiza Tume hiyo wafike kiwandani hapa mara baada ya kupata barua hiyo na kuchukua hatua nyingine za kisheria zifuate ,ili kutokomeza na kudhibiti watu wasio waaminifu wanaotumia nembo ya RSA”.
Akifafanua zaidi Kakunda amesema serikali haitamvumilia mtu yoyote atakayesababisha hasara kwa mwekezaji anayeendesha shughuli zake kiuhalali kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu wa sheria ya nchi.
Katika hatua nyingine Kakunda ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa shughuli wanazozifanya ikiwemo kutoa fursa za ajira kwa wazawa ambapo jumla ya watu 200 kutoka katika vyuo vya ufundi (Veta)wamepatiwa katika sekta tofautitofauti.
“Kiwanda hiki ni cha mfano hapa nchini ubunifu unaotumika hapa ni mafanikio makubwa sana katika sekta ya viwanda, anaunda vitu mbalimbali vya mabodi ya magari hususani katika soko la utalii kama tulivyoona, hivyo serikali inaunga mkono jitihada hizi na itachukua hatua dhidi ya watu waharibifu unaoendelea kulingana na mamlaka husika ,hatutapenda kiwanda hiki kirudi nyuma kamwe hivyo tutaendelea kutoa ushirikiano wenye tija na ufikie kiwango cha kutoa ajira kwa watu zaidi ya 1000 “.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Manmohan Bhamva amesema kiwanda chake kinakabiliwa na changamoto kubwa ya watu kuiga anachokifanya bila kufuata tarabu za kisheria na kuiomba serikali kusimamia jambo hilo kwa haraka zaidi ili kuboresha kiwango cha ubora na kuongeza soko la ushindani nje na ndani ya nchi na kufikia malengo ya kutoa fursa za ajira zaidi kwa wazawa.
“Tunashukuru leo ni mara ya kwanza umekuja kiongozi mkuu katika kiwanda chetu ,kwetu tunaamini hii yote ni kutokana na ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka serikalini katika Nyanja mbalimbali ,hivyo tunaahidi kuongeza ufanisi zaidi katika utendaji wetu”.
Hata hivyo baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wameeleza kunufaika zaidi kupitia ajira kiwandani hapo sambamba na kupatiwa mafunzo maalumu ya kiutendaji na kijikimu kimaisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Manmohan Bhamva akizunguza na Mh.Waziri mara baada ya kumpa viambatanisho mbalimbali juu ya umiliki halali licha ya kuwa kuwepo kwa watu wanaoghushi.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni