Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 7 Novemba 2016

JESHI LA POLISI MKOANI KILIMANJARO LAJIPANGA VILIVYO KUTOKOMEZA MADAWA YA KULEVYA.

KAMANDA WA POLISI MKOANI KILIMANJARO(RPC)WILIBROD MTAFUNGWA.


Kwa mujibu wa jeshi hilo kupitia kamanda wa mkoa (RPC) Wilibrod Mutafungwa amesema kulingana na kuwepo kwa vitendo mbalimbali  vinavyo ashiria uwepo wa biashara haramu ikiwemo uuzaji na uzalishaji wa gongo,madawa ya kulevya kama bangi,mirungi na mengineyo jeshi hilo limejipanga kuwabaini wahusika na kuwafikisha katika mikono ya sheria bila kujali vyeo ,nyadhifa mbalimbali .
Mbali na yote kamanda Mutafungwa amekua akifanya msako mkali katika kuwabaini wahusika na kulazimika kufanya mikutana mbalimbali na wananchi juu ya elimu ya uraia mwema na jeshi hilo kufanikiwa kukwakama wahalifu wa makosa mbalimbali ikiwemo ubakaji,ulawiti,ujambazi ,  uuzaji na usafirishaji wa madawa ya kulevya.
TIZAMA PICHA MBALIMBALI KATIKA WILAYA YA HIMO ZINAZOONYESHA JITIHADA HIZO.




Kamanda Mutafungwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya himo pamoja na wanafunzi wa shule saba za msingi , kuhusu elimu ya uraia mwema katika kuwabaini na kuwafichua wahalifu.
 

 Mutafungwa amesema"nilazima wazazi  tuanzie nyumbani katika kuhakikisha elimu inatolewa zaidi juu ya vitendo viovu katika ngazi ya shule za msingi na kuendelea, ili tuweze kufikia malengo ya kuwa na raia wema na kuongeza fulsa kwa wananchi  kutoa taarifa juu ya matendo ya kikatili wanayofanyiwa wanajamii".

  Kamanda Mutafungwaa anawaeleza wazazi na walezi kuwa na moyo wakukemea tabia mbalimbali  ikiwemo uzururaji ambao ni chanzo kikubwa kinachowafanya watoto kuhusishwa na biashara haramu mbalimbali ."wazazi wanapaswa kuwa na hofu ya Mungu na kuwalea watoto katika misingi ya imani ya dini".


ILI KUWA NA MAENDELEO THABITI LAZIMA WAZAZI TUJIKITE ZAIDI KATIKA MALEZI BORA.
 Hili ni taifa la kesho linalotakiwa kulelewa katika misingi mizuri na hatimaye kuwa raia wema katika kutekeleza majukumu ya kulijenga taifa.
 Baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi wakionekana katika picha....

 TAZAMA VIDHIBITISHO VIFUATAVYO IKIWA NI JITIHADA ZA JESHI LA POLISI KILIMANJARO KUTOKOMEZA UPIKAJI WA GONGO NA USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA .

 KAMANDA MTAFUNGWA (RPC)AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUWAONYESHA VIDHIBITI VYA WATUHUMIWA.

POMBE HII YA KIENYEJI IMEKUA IKIPEWA MAJINA MBALIMBALI KAMA CHANG'AA,MACHOZI YA SIMBA,NAMBA- 1,PANGA UZAZI,GONGO NA VUMILIA MWENDO.
WANAHABARI WAKITIZAMA KWA UMAKINI MADAWA YA KULEVYA WALIONYESHWA.
 
RUMBESA ZA MADAWA YA KULEVYA AINA TOFAUTITOFAUTI YALIYOKUA YANASAFIRISHWA.


 BAADHI YA WADAU WA HABARI WAKITETA JAMBO NA RPC MTAFUNGWA JUU YA UFAFANUZI.


TUWAFICHUE WANAFANYA BIASHARA HIZI HARAMU KUKOMESHA KABISA KILIMANJARO BILA MADAWA INAWEZEKANA.

KWA PAMOJA MIMI ,WEWE NA YULE TUTAWEZA KUOKOA RASILIMALI WATU NA TAIFA LA LEO.
CHUKUA TAHADHARI PIGA VITA USAFIRISHAJI NA BIASHARA HARAMU.
 KAMANDA MTAFUNGWA ANAWAONYESHA WADAU HAO KUHUSIANA NA NAMNA GANI WAALIFU WALIVYOSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA.
USAFIRI UNATUSAIDIA SOTE KAMA UTATUMIKA KWA MATUMIZI SAHIHI OKOA MAISHA YA WENGINE, JESHI LA POLISI LIPO MACHO KUTOKOMEZA BIASHARA ZOTE HARAMU.

UWENDAPO TUPO WANANCHI MSISHAWISHIKE JESHI LA POLISI LINACHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA.
WANAHABARI WAKIMUULIZA MASWALI TOFAUTI TOFAUTI RPC MUTAFUNGWA.
 RPC AKIWAONYESHA WANAHABARI NAMBA ZA USAJILI LA MOJA YA GARI ILIYOKAMATWA IKIWA IMEPAKIWA MADAWA YA KULEVYA.
TIZAMA HII!!! HUU SIO UZALENDO NI KOSA KISHERIA NA UKIUKWAJI WA MATUMIZI MABAYA YA USAFIRI.
WANAHABARI WAKISHUHUDIA NAMBA ZA USAJILI WA GARI LILILOKUA LIKITUMIKA KUSAFIRISHIA MADAWA YA KULEVYA.
 NGUVU KAZI YA TAIFA INAPOTEA KUTOKANA NA WATU WACHACHE KUJINUFAISHA NA BIASHARA HII HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA, MAMIA YA WATU WANAANGAMIA KUTOKANA NA HATHARI ZA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA.
   NA HAWA NI  WATUHUMIWA WA WASAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA WAKIWA CHINI YA ULINZI WA JESHI LA POLISI.

HATA HIVYO KAMANDA MTAFUNGWA AMETOA RAI KWA WANANCHI KUWARIPOTI WALE WOTE WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA UWALIFU,UVUNJIFU WA AMANI HARAKA PINDI WANAPOWABAINI NA JESHI HILO LITAWALINDA WATOA TAARIFA KWA WELEDI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni