Imeelezwa kuwa umahiri wa Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro
pamoja na uweledi katika kutoa na kupokea taarifa kutoka kwa raia wema
umefanikisha kuzuia matukio ya kiuhalifu wa kutumia silaha za moto.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani hapa Hamis Issah
amesema kupitia askari wa jeshi hilo wamefanikiwa kuzuia tukio la ujambazi kwa
kutumia silaa lililopangwa
kufanyika mnamo tarehe 08/10/2017 katika kijiji cha Chilio kilichopo kata ya
Holili Tarafa ya Mengwe wilaya ya Rombo katika kiwanda cha Moshi Cement.
Akifafanua zaidi kamanda Issah amesema jeshi hilo
lilifanikiwa kumtia mbaroni mmoja kati ya majambazi hao mnamo 05/10/2017 aliyejulikana
kwa jina la Robert Paulo Massawe (51)Mchaga mkazi wa Dar es salaam akiwa na
silaha aina ya Smg namba 1996AFU 2761 katika maeneo ya kaloleni karibu na
kiwanda cha ngozi na mara baada ya
kuhojiwa alikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya kiuhalifu na kuliahidi jeshi
hilo kulipa ushirikiano kwa kuwapeleka maeneo husika waliopanga kutimiza tukio
la kialifu na askari walilazimika kuunda mtego ili kuwadhibiti majambazi hao.
Issah amesema baada ya kufika eneo la tukio Massawe akiwa amesimama kwa ajili ya
kutekeleza uvamizi huo alipowakaribi wenzake aliwataarifu wenzake kwa kupiga kelele kuwa polisi wapo eneo hilo hali
iliyowapelekea majambazi hao kukimbia huku wakiwa wanapiga risasi ovyo kwa
lengo la kujihami wasikamatwe na kusabisha kifo chake kutokana na maumivu
makali ya risasi zilizompata maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo katika mkono wa
kushoto,mgongoni na mguu wa kulia.
Akitaja baadhi ya matukio ambayo alishawai kutekeleza wakati
wa uhai wake ni pamoja na 1991-1992 ambapo alikamatwa Tarekea wilayani Rombo
kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.
Mnamo 26/06/2012 katika maeneo ya Kyusa jirani na Panone
Petrol Station walimvamia mfanyabiashara na kumpora fedha ,29/9/2014 walimvamia
mfanyabiashara aitwaye Robart na kumpora fedha pamoja na vocha ,mnamo 26/6/2015
walivamia Holili stand na kumpora fedha mfanyabiashara mmoja na waliuwa watu
wawili,3/4/2017walimvamia mfanyabiashara mmoja maeneo ya Himo na kumpiga risasi
ya paja kasha kumpora fedha kiasi cha Tsh.million 6,27/4/2017 eneo la Osterbay
walimvamia mfanyabiashara akiwa dukani kwake na kumpiga risasi ya kichwa na
kumjeruhi mtu mwingine aliyekuwepo pembeni,26/6/2017 maeneo ya woodland
walimvamia mfanya biashara na kumpora simu yake pamoja na vocha na mnamo 22/7/2017
maeneo ya mailisita High way Supermarket walimvamia mfanya biashara na kumpiga
risasi ya paja kisha kupora simu pamoja na vocha za simu aina mbalimbali.
TIZAMA PICHA ZA KAMANDA WA POLISI MKOANI KILIMANJARO AKIWAONESHA WAANDISHI WA HABARI BAADHI YA VIELELEZO.
SIKILIZA SAUTI YA KAMANDA AKIELEZEA VIELELEZO HIVYO.
TIZAMA PICHA ZA KAMANDA WA POLISI MKOANI KILIMANJARO AKIWAONESHA WAANDISHI WA HABARI BAADHI YA VIELELEZO.
SIKILIZA SAUTI YA KAMANDA AKIELEZEA VIELELEZO HIVYO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni