Serikali ya Tanzania imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili zuio hilo pia linahusisha na kujumuisha machapisho ya mtandaoni.
Duru za habari zimesema kuwa chombo hicho cha habari kimefungiwa kwa kile kilicho arifiwa kuwa ni kuchapisha habari za
uongo na uchochezi ambazo zinadaiwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama
wa taifa hapa nchini .Mwanahalisi linakuwa gazeti la pili kufungiwa kwa kipindi cha miezi minne kwa tuhuma za
kuchapisha mlolongo wa habari ambazo zinasemekana kuwa ni za kichochezi ikiwemo yenye kichwa cha habari 'Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu' iliyochapishwa katika toleo la 409 la tarehe 18-24 Septemba 2017 .
Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikimulikwa kwa ukaribu nchini hapa kwa kile kinachodaiwa kuwa baadhi ya vyombo hivyo vinakiuka kanuni na taratibu wa tasnia ya habari na kuleta mkanganyiko unaolenga kuwapotosha wananchi na kuleta tafrani katika taifa.
Kama itakumbukwa mapema mwaka huu Raisi Magufuli alionya vyombo vya habari "visifikiri viko huru kwa kiwango hicho."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni