Watu wasiopungua
38,wengi wao wakiwa wanajeshi wameuwawa katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita kufuatia
mapigano makali kati ya jeshi la Libya na wanamgambo wa Kiislam katika mji wa
mashariki wa Benghazi-maafisa wa serikali wamesema.
Familia kadhaa zinayapa
kisogo maskani yao. Duru za kijeshi zimesema mapigano yameripuka jana pale
makundi ya itikadi kali yalipoyashambulia makao makuu ya kikosi maalum cha
jeshi karibu na eneo la kati la Benghazi na kusababisha hasara miongoni mwa
wanajeshi waliokuwa wakizihami kambi zao.
Hospitali kuu ya
Benghazi imesema miili 28 ya wanajeshi imepelekwa katika hospitali hiyo katika
kipindi cha masaa 24 yaliyopita,pamoja pia na majeruhi 50 huku miili ya
wanajeshi wengine 2 na majeruhi 10 wakipelekwa katika hospitali ya Al-Marj
iliyoko kilomita 100 mashariki ya Benghazi. Msemaji wa baraza la
mapinduzi-linaloyaleta pamoja makundi tofauti ya itikadi kali amesema
wamewapoteza wapiganaji wao wanane.
Baraza la mapinduzi
linadai kuhusika na mashambulio kadhaa katika eneo hilo la mashariki ya Libya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni